RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kitendo cha timu za Taifa kufungwa anatamani siku moja awe Waziri wa Michezo ili apange timu mwenyewe.

Magufuli amesema huwa anaumia sana na  ameboreka kwa kitendo cha timu ya Taifa ya Vijana, Serengeti Boys kufungwa mabao mengi katika ardhi ya nyumbani.

Akizungumza leo wakati wa hotuba mbele ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wilayani Kyela, Magufuli amesema hajafurahishwa na timu ya vijana kufungwa mabao mengi tena wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani na mashindano wakiwa wameandaa wenyewe.

"Hii ni aibu kwa Taifa, tupo milioni 55 tukifungwa tunaaibika wote haiwezekani Waziri unaangalia tu labda kufungwa ni mchezo mzuri, mashindano tumeaandaa wenyewe, uwanja wa kwetu wenyewe, tumefungwa mabao mengi kwelikweli, hili ni jambo la ajabu ungechukua hata timu ya Kyela tusingefungwa hivi, " amesema Magufuli.

"Sasa hili linapaswa liangaliwe kwa usawa, ninatamani siku moja niwe Waziri wa Michezo na nikiwa Waziri wa Michezo timu nitaipanga mwenyewe, na timu nyingine hiyo nayo inajiandaa sijui na wao watapigwa kama hawa,"

Michuano ya Afcon ambayo imemalizika wikiendi hii, Cameroon imebebwa ubingwa kwa vijana, huku Tanzania ikitolewa na zigo la mabao 12 ya kufungwa na imefunga mabao sita pekee kwenye michezo mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...