*Akumbuka simu aliyopigiwa saa nane usiku akipewa maagizo ya ujenzi Mji wa Serikali

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dk.John Magufuli halali kwasababu ya kuwaza kuwaletea maendeleo ya Watanzania wote huku akifafanua amekuwa akipokea simu za Rais hadi saa nane usiku.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Aprili 13,2019 wakati anazungumza kwenye uzinduzi wa Mji wa Serikali Dodoma ambapo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na maendeleo na kubwa zaidi ni uamuzi wa Rais wa kutoa tamko la kuhamishia Serikali Dodoma na hatimaye ndoto hiyo imetimia.

"Rais wetu unafanya kazi kubwa sana kwa ajili ya nchi yetu,naomba niseme kitu,kuna siku Rais ulinipigia simu saa nane na dakika 25.Nimetaja hizi dakika kwasababu baada ya kuangalia saa nikaona ni saa nane,nikaamua kuangalia dakika ni 25.Ilikuwa usiku wa maneno Rais yuko macho.

" Nilichojifunza ni kwamba Rais wetu halali kwa ajili ya kuwaza maendeleo ya nchi yetu,nakumbuka siku hiyo ulitoa na maelekezo kuhusu ujenzi wa Mji wa Serikali na baada ya hapo tukaanza utekelezaji wake na leo hii unazindua Mji wa Serikali hapa Dodoma .Ahsante Rais na nikuahidi tutaendelea kupokea maagizo yako na tutayatekeleza kwa wakati,"amesma Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesisitiza kila ambacho Rais ataagiza watatekeleza na kutumia nafasi hiyo kuwaomba watumishi kutozima simu zao kwani maagizo na maelekezo yanaweza kutolewa wakati wowote na yanahitaji kufanyiwa utekelezaji wa haraka.

Akizungumzia majengo hayo ya Serikali,Waziri Mkuu amesema majengo 20 tayari yamekamilika na baada ya kuzinduliwa leo na Rais watumishi wataanza kutoa huduma kuanzia kesho na kufafanua watumishi wote walilloko Dodoma watakuwa huko.

Pia amesema kuna baadhi ya majengo ujenzj unaendelea na upo katika hatua.mbalimbali na hiyo imetokana na aina ya ramani ya jengo lakini akafafanua kuwa nayo yatakamilika katika kipindi kifupi kuanzia sasa. 

"Kuanzia kesho watumishi wote watatoke Ihumwa katika Mji wa Serikali kwani walikuwa wanasubiri kufanyika kwa uzinduzi na huduma zote muhimu zipo ikiwemo maji ,umeme,barabara za lami na kinachoendelea ni mtandao wa mawasiliano," amesema Waziri Mkuu.

Akifafanua zaidi kuhusu kuhamishiwa Serikali Dodoma amesema inatokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo imezungumzia kufanyika mchakato wa Serikali kuhamia Dodoma na kisha Rais Magufuli katika kutekeleza hilo alitangaza rasmi kuanza utekelezaji ambao sasa umetimia.

Pia amesema kutajengwa kituo cha afya katika eneo hilo la Mji wa Serikali ambacho kitatoa huduma kwa watumishi wa umma waliko maeneo hayo na wananchi kwa ujumla.Amefafanua kuwa kukamilika kwa Mji wa Serikali Dodoma kunakwenda kufungua fursa nzuri za ajira kwa wananchi ambapo zaidi ya wananchi 1000 wa mkoa huo wamepata ajira.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akiteta jambo na Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, kwenye uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma Aprili 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa taarifa ya Serikali kuhamia Dodom, kwenye uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma Aprili 13, 2019. Mgeni rasmi alikua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...