* Amwomba Rais Magufuli kukabidhi mradi wa nyumba  uliodumu tangu mwaka 2004 kwa wanajeshi huko Tuangoma, Temeke

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za askari Magereza na Maafisa katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam mradi ambao ameridhishwa nao.

Akizungumza mara baada ya kukagua majengo hayo kumi na mbili Makonda amesema kuwa huo ni muendelezo wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jijini humo, amesema kuwa ilidhaniwa kuwa Wizara husika zinasimamia miradi lakini la hivyo ataendela kukagua miradi yote ya kimaendeleo ndani ya Mkoa huo.

Aidha amempongeza Mkuu wa operesheni hiyo Brigedia Jenerali Charles Mbuge kwa usimamizi bora wa mradi huo ambao ulikabidhiwa kwa jeshi la wananchi na Rais Dkt. John Magufuli  Machi 16, mwaka huu baada ya Wakala wa majengo nchini (TBA) kushindwa kusimamia mradi huo ipasavyo.

Makonda amesema kuwa Mbuge amekuwa kiongozi mzalendo na mfuatiliaji wa majukumu yake, na kueleza kuwa kabla ya kwenda Mererani aliacha ofisi 50 za walimu alizokuwa anazisimamia katika hali nzuri sana na amewataka wafanyakazi wa serikali kufanya kazi kwa bidii na kuiga mfano kutoka kwa wanajeshi kwa uchapakazi na uzalendo.

Wakati huo huo RC Makonda amemuomba Rais Dkt. John Magufuli kuangalia mradi wa nyumba nyingi zilizopo Toangoma katika Manispaa ya Temeke mradi unaotekelezwa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF.

Makonda amesema kuwa mradi huo umeanza tangu mwaka 2004 na bado haujakamilika na amemwomba Rais Magufuli kukabidhi nyumba hizo kwa jeshi la wananchi na ukikamilika aelekeze kwa watu wa kuzitumia kwa kuwa yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Akitoa maelezo ya mradi huo Mkuu wa operesheni hiyo Brigedia Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa mradi huo wa nyumba za kikosi cha Magereza ulikabidhiwa kwao na Rais Dkt. John Magufuli Machi 16 mwaka huu na ndani ya miezi miwili na nusu utakuwa umekamilika.

Amesema kuwa mradi huo unatekelezwa na wanajeshi wa jeshi la wananchi kwa kushirikiana na wafungwa 33 walio chini ya maafisa wao.
 Muonekano wa nyumba hizo pamoja na wanajeshi wa jeshi la wananchi ambao wapo  kazini katika kutekeleza mradi huo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishiriki shughuli ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza Ukonga, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa operesheni ya mradi huo Brigedia Jenerali Charles Mbuge (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda juu ya mradi huo wa ujenzi wa nyumba za askari wa jeshi la Magereza Ukonga, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa jeshi wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari wa jeshi la Magereza katika gereza la ukonga, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...