NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemkabidhi bajaj iliyogharamiwa kiasi cha sh.milioni 7.9 ,mlemavu aliyekatwa miguu miwili kutokana na kuugua ,Domitian Magomba .

Bajaj hiyo ni msaada kutoka kwa mfanyabiashara ,Reginald Mengi,ambae ofisi ya mkoa huo ilimuomba msaada ili amsaidie mzee huyo.

Akikabidhi bajaj hiyo, mhandisi Ndikilo amesema kabla hujafa hujaumbika kwani Magomba alizaliwa mzima na akiwa shule ya sekondari alikuwa mchezaji mpira. 

Alieleza,mzee huyo hakutaka kuendelea kupewa misaada ya fedha kila siku kwakuwa anahudumia familia ndipo alipokwenda ofisini kwake kumuomba msaada huo. 

"Hakukata tamaa kwakuwa anafamilia alikuwa akijakuomba msaada kwangu na baadae akaona aombe msaada wa kimaendeleo, apewe mtaji, nikaongea na mdau Reginald Mengi na nashukuru alikubali ombi hili na kuamua kutoa fedha hizo "alisema Ndikilo. 

Hata hivyo Ndikilo alimkabidhi sh. 150,000 mzee huyo ili imsaidie katika mwanzo wa biashara yake kama kuweka mafuta. Akikabidhiwa msaada huo, Magomba aliishukuru serikali ya mkoa wa Pwani kwa kusikiliza shida za watu wenye mahitaji maalum pamoja na kumshukuru Mengi kwa kusaidia. 
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...