Na Vero Ignatus, Arumeru. 
Mkuu wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewahakikishia wananchi wa Arumeru kuwa wataendelea kutatua kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo migogoro ya Ardhi.
Ameyasema hayo wakati akimtambulisha RPC mpya wa mkoa wa Arusha Jonathan Shanna alipotembelea ofisini kwake leo na kuzungumza na wananchi. 

Jerry amesema ofisi yake imeweka mkakati wa kuwasaidia wananchi kwa kuwaajiri wanasheria wanne ambao anawalipa kwa kutoa sehemu ya mshara wake kwaajili ya kuwasaidia  wananchi wasiokuwa na uwezo wa kupata haki zao. 


Wakati huo huo RPCJonathan Shanna  amemuagiza mkuu wa polisi wilaya Arumeru  SSP Hamisi Mwampelwa, kumsimamisha kazi  mara moja mkuu wa kituo cha polisi Kikatiti Inspector Michael Magere kwa kushindwa kusikiliza kero za wananchi wanapo kituoni hapo

Shanna akizungumza na wananchi wa Arumeru amewahakikishia kuwa atawaondoa askari ambao watakiuka taratibu wa jeshi la polisi bila kujali cheo alichonancho. 

 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wananchi wa Arumeru na kumtambukisha RPC mpya mkoa wa Arusha kwa wananchi wa Arumeru ambapo alipata pia nafasi ya kusikiliza kero za wananchi ikiwemo ya Ardhi. Picha na Vero Ignatus. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akizungumza mara baada ya kutambulishwa kwa wananchi wa Arumeru na mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro. 
 Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akizungumza na wananchi wa Arumeru (hawapo pichani) mara baada kusikiliza changamoto zinazohitajika kutatuliwa na Jeshi la Polisi katika wilaya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...