NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, limepiga marufuku kupiga disko toto
pamoja na kuwaasa wamiliki wa kumbi za starehe kuacha kujaza watu
wengi kuzidi uwezo wa kumbi zao, kwenye sikukuu ya pasaka.
Aidha limejipanga kufanya msako na doria ili kuhakikisha hakuna tukio
la kihalifu litakalofanikiwa kuelekea sikukuu hiyo.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa aliwatahadharisha,
wamiliki hao kuzingatia sheria na atakaekiuka agizo hilo hatua
zitachukuliwa dhidi yao.
Katika hatua nyingine ,aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto
kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuzuia ajali katika
barabara za mkoa huo.
Wankyo alisema, madereva wasiendeshe baada ya kutumia vileo kwani
askari wao wa kikosi cha usalama barabarani wapo kila kona hivyo
hawatoweza kupita mkoani humo,pasipo kukaguliwa .
"Kwa wamiliki wa magari yanayosafirisha abiria kuzingatia uwepo wa
madereva wawili na magari yatakayobainika kuwa na dereva mmoja
hayataruhusiwa kuendelea na safari"
Kamanda huyo hakusita kuwaomba wazazi na walezi kuweka ulinzi
majumbani mwao endapo watatoka kwenda kwenye nyumba za ibada na
kuwawekea waangalizi watoto watakapowaacha nyumbani.
WAKATI HUO HUO, jeshi hilo linamshikilia Mwamini Shomary (37) ,mkazi
wa Yombo Bagamoyo kwa kosa la kusafirisha mafuta ya kula dumu kumi
yenye thamani ya laki tano, ambayo hayajalipiwa ushuru.
"Askari wetu wakiwa doria maeneo ya Kwamatias, huko Kibaha walimkamata
mtuhumiwa akiwa na mafuta hayo aina ya mico gold ujazo wa lita 20 kila
moja akitokanayo Bagamoyo.
Wankyo alielezea kwamba, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazomkabili.
Kamanda huyo aliongeza kusema, pia wamekamata bangi puli tano, kete
155 na pombe aina ya gongo lita 11.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...