Wenyeji wa mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON)  kwa chini ya vijana wa miaka 17 timu ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ wameondoshwa kwenye mashindano hayo wakiwa na alama sifuri. Serengeti Boys Wamemaliza kundi A wakiwa hawajafanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wowote kati ya mitatu waliyoicheza.

Kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Angola Serengeti Boys walihitaji ushindi wa goli 4-0 na kumuombea Uganda apoteze mchezo wake dhidi ya Nigeria.

Katika mchezo wa leo, Serengeti Boys ndio wa kwanza kuliona lango la Angola katika dakika ya 12 kupitia kwa beki wake Omary Omary aliyeandika goli la kwanza akimalizia kona safi kutoka upande wa kushoto.

Vijana wa Serengeti wakiendelea kusaka goli lingine, ilichukua dakika 5 kwa Angola kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa beki wake wa kati Mimo kwa kichwa .


Dakika ya 41,Omar anamfanyia madhambi mchezaji wa Angola na mwamuzi kuweka tuta’ mkwaju wa penati’ na kufanikiwa kuandika goli la pili na katika dakika ya 43 Agiri Ngoda anaisawazishia timu yake na kwenda mapumziko wakiwa 2-2.


Kipindi cha pili kilianza kwa kila upande kusaka nafasi ya kupata goli la ziada, na katika dakika ya 62  Mchezaji wa Angola Davidi anaiandikia timu yake goli la tatuna Mfungaji wa goli la pili Capita  anaiandikia timu yake goli la nne na kuzizima ndoto za watanzania kwenda kombe la Dunia la Vijana nchini Peru mwaka huu.

Baada ya matokeo hayo, Serengeti Boys wanapoteza mchezo wa tatu kwa jumla ya magoli 12 wakifungwa 5-4 dhidi ya Nigeria, 3-0 na Uganda na 4-2 kwa Angola.


Kwenye mchezo mwingine wa kundi B, Nigeria na Uganda wanatok sare 1-1 na kuipa nafasi Angola kuungana na Nigeria kwenda hatua inayofuata akiwa nyuma ya Nigeria wenye alama 7 na Angola akiwa na alama 6.

Mechi zingine za kundi B zitachezwa hapo kesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...