WAZIRI
wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Januari
Makamba amesema kwamba katazo la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki
nchini litakuwa la kisheria na kanuni zake zitakazokuwa na adhabu kwa
wale watakaokiuka.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Makamba pia amesema katika kipindi hichi cha
mpito,wizara yake itaweka utaratibu wa mahali pa kuiweka,sehemu ya
kuisalimisha na kuiteketeza kwa walio na mifuko hiyo katika magodauni
yao kabla haijawa kosa kisheria kwa muda uliowekwa na Serikali.
Kwa
kukumbusha tu,mapema wiki iliyopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa
bungeni Mjini Dododma,alisema kuanzia Juni Mosi mwaka huu, itakuwa ni
marufuku kutengeneza, kuuza, kuingiza na kutumia mifuko ya plastiki kwa
ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote.
Hivyo
Waziri Makamba wakati anazungumza na wadau wa mifuko ya plasiki, kuhusu
fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki
amefafanua katazo hilo litakuwa la kisheria na sio tamko.
Ameongeza
kuwa katazo hilo ni kuanzia uzalishaji, kuuza, kuingiza, kumiliki,
kuhifadhi kutumia,yote hayo ni makosa.Kanuni hizo watakazoweka zitakuwa
na adhabu kwa watakaokiuka hata atakayekutwa naye na kutakuwa na faini
au vifungo kwa mujibu wa sheria,kanuni zitakapokamilika
zitatangazwa"alisema Makamba
Pia
amesema katazo hilo halitausisha vifungashio vya plastiki kwa bidhaa
kama Korosho,maziwa, na nyinginezo bali litaanza kwa mifuko ya plastiki
inayotumika kubebea bidhaa.
Wakati
huo huo Makamba amesema uwamuzi wa katazo hilo si wa gafla kama
inavyosemwa na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya kutengeneza mifuko ya
plastiki kwani inafahamika tangu Agosti mwaka 2016 kwa wadau kuandikiwa
barua kujadili kupiga marufuku mifuko hiyo.
Makamba
amesema katazo hilo lina manufaa kwa taifa kàtika kutunza mazingira na
kwamba kwa mwaka mifuko bilioni 3 inaishia katika fukwe za mito,bahari
na kukaa muda mrefu ikichafua mazingira.
Kwaupande
wake ,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amewataka
watakaopewa mamlaka ya kusimakia katazo hilo kutolichukulia kama fursa
ya kuomba na kupokea rushwa.
Kwa
baadhi ya mawakala na wafanyabiashara wa mifuko ya plastiki kutoka
Sokoni Kariakoo wameiomba serikali iwaongezee muda wa kuiuza hadi
Januari mwakani, kwani bado ipo mingi na wanadaiwa na wafanyabiashara
raia wa china waliowapa.
Hat
hivyo,Waziri Mahakama akijibu hoja hiyo,alisisistiza kuwa katazo hilo
ni msimamo wa Serikali na halitarudi nyuma hivyo wakae na waliowauzia
kuona kama watawalipa fidia ama la.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...