Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira mazuri Kwa watoto nchini Kwa lengo la kuondoa changamoto wanazokumbana nazo.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa ya Themi wakati wa maazimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto yaliofanyika jijini Arusha na kusema kuwa ndio maana serikali ikaanzisha huduma bure ya elimu nchini.

Ameeleza kuwa kumekuwepo na mikakati mbali mbali iliyoandaliwa na serikali Kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na wanaofanyakazi mitaani ikiwa ni lengo la kuwaunganisha na familia zao na jamii kuweza kufikia malengo yao ikiwemo kusoma na kupata matibabu sanjari na makazi.

Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha Martha George alisema jiji la Arusha limeweza kuwaunganisha watoto waishio mitaani na mazingira hatarishi katika vituo vya kulea watoto hao na wengine kuwarudisha katika familia zao.

Amesema kuwa malengo ya maadhimisho hayo ya kila mwaka yamejikita kuhakikisha kuona umuhimu wa kuisogeza jamii kuwalea watoto wenye uhitaji na wanaoishi na kufanyakazi mitaani.

Kwa upande wao watoto hao kwenye Risala yao wamesema kuwa wanakumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo kutopata elimu sanjari na malezi Bora na kuiomba serikali kuona umuhimu wa kuwaunganisha na familia zao.

Wameeleza kuwa changamoto hizo ni pamoja na jamii kuwanyanyapaa na kuwaona sio sehemu yao Kwa kuwaita majina mbali mbali hivyo kuiomba jamii kuwaona ni sehemu ya maisha yao.

Jumla ya watoto 6,393 Sawa na asilimia 76 wanaishi katika mazingira hatarishi kwenye majiji sita hapa nchini hii imebainishwa na ripoti ya wizara ya afya kwenye mpango wa kizazi kipya Kwa ushirikiano na USAID.

Ambapo watoto wenye umri Kati ya miaka 15-18 Sawa na asilimia 51 huku watoto wenye umri wa miaka 11-14 wakiwa Sawa na asilimia 35 huku ikionyesha watoto wenye umri 0-10 Sawa na asilimia 14 huku watoto wakike wakiwa Sawa na asilimia 86 kwenye umri unaonzia miaka 15-18 

Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi yaliofanyika jijini Arusha yenye kauli mbiu ya "hakikisha usawa Kwa watoto wote" Kwa kuwapatia ulinzi na mahitaji yote Kwa watoto wenye kuishi katika mazingira hatarishi.

Ugumu wa kurudi shuleni uksefu wahali ya upendo vipigo bajeti za watoto wenye kuishi mtaani Kwa kurowabaguza kwani sikuhiini muhimu Kwa kuikumbusha serikali umuhimu wa matunzo ya watotowanaoishi katika mazingira hatarishi.

Jiji la Arusha Lina jumla ya watoto 544 wanaofanyakazi katika kada mbali mbali kama ripori ya serikali inavyoonyesha ambapo watoto hao wanatoa wito Kwa wadau kuwaona kama jamii na kuwasaidia ili nao waje kuwa mfano katika jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...