Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Harusi Suleiman amezitaka Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- na Mnazi Mmoja kudumisha uhusiano na ushirikiano uliopo ili kuwaenzi waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Naibu Waziri Suleiman ametoa kauli hiyo katika hafla ya kuhitimisha tamasha la Pasaka   2019 lililofanyika Visiwani Zanzibar na kuhusisha timu za michezo za Muhimbili pamoja na Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo visiwani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo amesisitiza kwamba timu hizo zimekuwa zikikutaka kila mwaka kwa lengo la kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya pande hizo mbili ambapo mwaka jana tamasha hilo lilifanyika Tanzania Bara. “Ndugu zangu tumefarijika kuja kututembelea katika pasaka hii tunaomba ushirikiano huu uendelezwe kwa faida ya pande zote mbili, pia kikubwa nilichofurahishwa kutoka kwenu ni nidhamu pamoja na maadili kwani hata katika michezo tunasisitiza nidhamu na maadili hakika mnastahili pongezi”. Amesema Naibu Waziri wa Afya Zanzibar.

“Lakini pia yapaswa kuwashukuru viongozi wetu ambao walianzisha muungano wetu ambao umetuwezesha kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo michezo hivyo hatuna budi kuwaenzi kwa kuendeleza na kuiboresha zaidi michezo hii ambayo ilianzishwa mwaka 1972”. Amesisitiza Mh. Suleiman.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi kutoka Muhimbili Dkt. Praxeda Ogweyo, amewapongeza wanamichezo wote walioshiriki katika tamasha la Pasaka 2019 na kueleza kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha michezo inaendelezwa katika taasisi hiyo na kutoa fursa kwa watumishi wengi kushiriki.
Naibu Waziri wa Afya Mh. Harusi Suleiman akizungumza na wanamichezo katika hafla ya ufungaji wa tamasha la pasaka liliofanyika Zanzibar na kuhusisha timu za Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo, akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga tamasha hilo.
Baadhi ya wanamichezo wakikiliza neno kutoka kwa Naibu waziri wa Afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...