Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii 

*Kutangaza Utalii wa Tanzania 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameipongeza SportPesa kwa kufanikisha ujio wa timu hiyo na kueleza kuwa kampuni ni mdau mkubwa wa michezo nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma leo, Shonza amesema ujio wa Sevilla nchini utaitangaza Tanzania duniani na hivyo kusaidia kuwatangaza hata wachezaji wa Tanzania watakaocheza dhidi ya timu hiyo Mei 23. "Hivi sasa, Tanzania imeanza kuonesha mafanikio makubwa katika mchezo wa soka na michezo mbalimbali na kutia imani kwa wananchi kwamba pale tunapotaka kufika, itawekana," amesema.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangalla, ameipongeza SportPesa kwa kuamua kuwaleta Sevilla Tanzania, amesema wizara yake itautumia ujio wa timu hiyo kama fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. 

Amesema timu hiyo itakapowasili nchini, wataipeleka kwenye hifadhi moja au mbili kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii nchini. "Tunaamini kwa kufanya hivi tutaongeza idadi ya watalii. Tutaangalia pia uwezekano wa kuwapeleka Zanzibar kutembelea fukwe," amesema.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Ndugu Tarimba Abbas amesema ziara hiyo ni muendelezo wa ahadi ya kampuni hiyo ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.

“SportPesa inapenda kuendelea kushirkiana na La Liga ambayo inatajwa kuwa Ligi bora duniani ili kuvinadi vipaji vilivyopo nchini pamoja na kukuza kiwango cha soka nchin.
Picha ya Pamoja kati ya Kampuni ya Kubashiri ya Sportpesa na Viongozi wa Serikali, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangalla na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. 

Ikiwa nchini Tanzania, Sevilla FC ambao wanagombea nafasi ya kushiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao, watashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

Muendelezo wa historia “Mwaka 2017 dunia ilishuhudia klabu ya Everton ikitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza na muitikio ulikuwa ni wa kipekee. Hivyo tukaona umuhimu wa kuendeleza historia hiyo kupitia ushirika na LaLiga

“Kutokana na kuwa na ushirika na taasisi kubwa za soka duniani, tukaona basi ni vyema kuendeleza kuleta msisimko wa soka nchini Tanzania wenye hadhi sawa na ule wa Everton kwa kuileta timu ya Sevilla nchini Tanzania ambayo ni moja ya vilabu bora barani Ulaya kwa kushirikiana na wenzetu wa LaLiga,” alisema Ndugu Tarimba

“Lengo ni kuionesha dunia kuwa Tanzania ni mahala sahihi kwa vilabu vikubwa duniani kuja kwa ajili ya ziara za maandalizi ya Ligi bila kusahau kuvinadi vipaji adhimu vya soka vilivyosheheni nchini”.

Mwaka juzi, Kampuni ya SportPesa ilifanikisha ujio wa timu ya Everton inashiriki Ligi Kuu ya England (EPL). Ikiwa nchini, Everton ilikipiga dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...