Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ni Sheria ya kimapinduzi ambayo ilikuja nchini kwa wakati muafaka na kufafanua kuwa anaiona sheria hiyo kuwa ni ya kimapinduzi kwa kuwa nchi nyingi duniani zimeshindwa kuwa na Sheria kama hiyo.

Prof. Kabudi amesema hayo bungeni jana wakati alipokuwa akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wake Dkt. Augustine Mahiga.

“Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ni Sheria ya kimapinduzi na nchi nyingine mpaka leo zimeshindwa kutunga sheria ya aina hii, ilikuja kwa wakati muafaka na ni ya kimapinduzi kwa kuwa watu wengi wameshindwa kuwa na Sheria kama hiyo,” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi aliongelea suala hilo baada ya wabunge waliokuwa wakichangia hoja ya Dkt. Mahiga kutaka Sheria hiyo ya Ndoa ifanyiwe marekebisho hasa katika kipengele cha umri wa mtoto  wa kike kuolewa.

Amewataka Wabunge waache kuchukulia kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa kama kigezo cha kuifanya sheria hiyo kuwa mbaya na kwamba yapo mambo maengi mazuri ndani ya sheri hiyo kama vile muwezesha mwanamke alieolewa kumiliki mali huku akitumia jina la baba yake , enzi za ukoloni jambo hilo lilikuwa haliwezekani.

“Tusichukulie suala moja tu kuwa ndio kigezo cha kusema sheria hii  ni kandamizi, kifungu hicho cha umri wa kuoa au kuolewa hakizungumzii msichana tu bali pia kinazungumzia mvulana, ndani ya sheria yetu wako wavulana wanaoweza kuoa chini ya umri mdogo, sheria hii ni sheria ya kimapinduzi kwasababu ni sheria kwanza iliyowakomboa wanawake wa kitanzania hasa wenye ajira, kwa kuweza kwenda kufanya kazi na kutpanda vyeo kwa sababu kabla ya hapo Sheria tuliyoachiwa na Muingereza ilikuwa inasema mwanamke lazima akae mahali alipo mmewe na hili liliwanyima wanawake fursa,” alifafanua Prof. Kabudi.

 Amesema kuwa umri wa mtoto wa kike kuolewa ni jambo nyeti sana na litasababisha ugomvi hata miongoni mwa wabunge kwani hata nchi zilizoendelea akiitolea mfano Uingereza umri wa mtoto wa kike kuolewa ni miaka 16 na kuongeza kuwa wasichana hawaolewi kwa sababu ya fursa mbalimbali za elimu na mwamko.

Amewataka wabunge kuisoma vizuri sheria hiyo kwani ina mambo mengi mazuri ambayo imeyaweka n ani makubwa hivyo ni vizuri tukaielewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...