Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV,  Bukoba.
Timu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club imewasili salama katika Manispaa ya Bukoba mapema Ijumaa Aprili 19, 2019 tayari kwa Mchezo wao na Wenyeji Timu ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumamosi hii Uwanja wa Kaitba.
Baada ya Kupokelewa na mashabiki ndakindaki na wanazi pamoja na viongozi wa matawi ya Kalbu hiyo,majira ya saa nne asubuhi Uwanja wa ndege wa Bukoba, Timu ya Simba Imesindikizwa kwa msafara wa magari na bodaboda hadi hotelini (STELLA HOTEL) maeneo ya Kashura ambapo Klabu hiyo itakuwa hapo kwa mapumziko na baadae  itafanya mazoezi mepesi Uwanjani kaitaba majira ya mchana.
Mchezo wa kesho Kati ya Simba na wenyeji Kagera Sugar ni mchezo wa 152 mzunguko wa  kwanza (kiporo)  mchezo ambao ni  muhimu sana kwa Timu zote mbili wakati Simba ikiwa katika mbio za Ushindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kagera wao wakiwa mbioni kutetea nafasi ya kutoshuka daraja, kwani kwa mechi sita zilizosalia Timu hii ya Kagera Sugar inatakiwa kuvuna pointi sita ili isiweze kushuka daraja.
Waamuzi wa mtanange huo hapo kesho, ni pamoja na Jacobo Adongo (Mara), Ferdinand Chaha (Mwanza), Joseph Matija (Mwanza), na Ahmada (Kagera).

 Shabiki wa Kagera Sugar, akikatiza mitaa mbalimbali ya Bukoba Manispaa kuwapa hamasa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kuipa nguvu watapopepetuana na Simba leo uwanja wa Kaitaba
 Shabiki wa Simba Bi Rehema Ngelekule akiongea na Michuzi TV juu ya mtanange huo
 Mtoto Eligius Erasto (6) anasema kajiandaa vyema kuishangilia timu yake
 Simba wakiwasili Bukoba
 Mshambuliaji Meddie Kagere na mshabiki wa Simba Eligius
 Mashabiki wa Simba wakisindikiza basi la wachezaji kuelekea Stella Hotel
 Mashabiki wa Simba wakisindikiza basi la wachezaji kuelekea Stella Hotel

 Mashabiki wakiwa wamejipanga maeneo ya Kashura ilipo Stell Hotel

 Msafara wa Simba wakielekea mazoezini uwanja wa Kaitaba
 Wachezaji wa Simba wakiwa uwanja wa Kaitaba wakijiandaa  tayari kwa mtanange wao na Kagera Sugar leo jioni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...