Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanawake Wahasibu nchini baada ya kufunga Mkutano wa Pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu(TAWCA)
Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akikabidhiwa vipeperushi vya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) baada ya kufunga mkutano wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini(TAWCA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.TANESCO ndio waliofanikisha kufanyika kwa mkutano huo kwa kuamini utaleta tija katika maendeleo ya nchi hasa kwa kuzingatia ulilenga kuwajengea uwezo wanawake wahasibu
 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SPIKA wa Bunge mstaafu Anne Makinda amewataka Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini( TAWCA)kujiamini,kuthubutu na kuwa na mtandao katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendelo nchini.

Pia amewakumbusha TAWCA wahakikishe wanawajali wanawake wa hali chini kwa kuwajali na kuwasaidia kufanikisha ndoto zao pamoja na kuwaonesha upendo.

Makinda ameyasema hayo wakati anafunga Mkutano wa Pili wa TAWCA ambapo mkutano huo umefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam .Wahasibu wanawake wa TAWCA wameshiriki mkutano huo.

"Niwapongeze sana TAWCA kwa namna ambavyo mmejadili mambo yenu na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo mlipokuwa kwenye mkutano wenu kupitia mada ambazo zimetolewa.Kwa namna ambavyo mmejipanga na kwa mikakati yenu mtafika mbali sana.Ni wanawake wenye utalaam wenu ambao mnapanga mambo yenu na yanapangika.Hongereni sana," amesema.

Makinda ametumia nafasi hiyo kueleza wanachama wa TAWCA wana kilasababu ya kujiamini katika kufanya mambo ya maendeleo katika jamii yetu na kwamba pamoja na mambo mengine watambue kupanga muda katika kufanya jambo lolote ni jambo la msingi na lenya maana.

"Hakikisheni suala la muda mnalipa kipaumbele kinyume na hapo mambo hayatakwenda sawasawa.Muda ni muhimu katika kupanga maendeleo,pia tengenezeni mtandao ambao nao ni muhimu kwani huwezi kufanya maendeleo peke yako," amesema Makinda.

Kuhusu TAWCA kuwajali wanawake wengine na hasa wale wanaonekana wa hali chini,Mama Makinda amesema ni muhimu wanawake wa chini wakaoneshwa upendo kwani humsaidia kumpa faraja na kubwa zaidi kuhakikisha wanabeba ndoto zao na kuzifanyia kazi.

Wakati anazungumzia wanawake wa hali ya chini,ametoa mfano kwa wadada wanaofanya kazi za ndani ambapo amesema ni muhimu wakathaminiwa badala ya kuzarauliwa na wenye nyumba kisa tu anafanyakazi katika nyumba yako.

"Tuishi vizuri na hawa wanawake(wadada wa kazi) ambao tunaishi nao majumbani.Kwangu mimi huwa nashindwa kumuita dada wa kazi maana naona sitatenda haki.Hivyo Wanawake wahasibu na wanawake wengine kwa ujumla tambue thamani ya hao wadada.

" Wapendeni na kubwa zaidi hakikisheni mnatimiza ndoto zao kwani pamoja na kuwa wanafanya kazi za ndani nao kuna ndoto wanazo.Ukipenda dada wa kazi na kumjali hata ulinzi wa nyumbani mnaongezeka.Unaporudi nyumbani rudi na zawadi ya dada ,atakupenda na atafanya kazi zake kwa bidii,"amesema Makinda.

Kuhusu TAWCA ,Makinda amewema amefurahishwa na namna ambavyo wanawake wahasibu ambavyo wamejipanga kuhakikisha wanatimiza malengo yao na kwa mtazamo wake watafika mbali kikubwa ni kuyasimamia yale ambayo wanakubaliana na kuyaamua kupitia vikao vyao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) Neema Kiure-Mssusa amesema kikao chao cha siku mbili kimekuwa na mafanikio nakubwa,hivyo kikubwa ni kuyatekeleza kwa vitendo yote ambayo wamekubaliana kama maazimio.

"Kikao chetu kimepata mafanikio makubwa,ndugu washiriki tukayafanyie kazi ambayo tumekubaliana.Pia tuwahakikishie tutaandaa notisi na kisha kuzisambaza kwa wanachama wetu kwa lengo la kukumbusha ambayo tumejadiliana.

" Niwahakikishie yale ambayo yanahitajika kutekelezwa lazima yatekelezwe kwa wakati. Na niwaombe huu ni wakati wa kuendelea kusoma,lazima tusome kwa bidii ili kuongeza maarifa.Kwa kuwa hatusomi hata watoto wetu wakiulizwa wanasema mama hasomi ila afanya kazi.Anajibu hivyo kwasababu hawatuoni tukisoma,hivyo tusome,"amesema.

Ameongeza wanatambua TAWCA wana maono yao mengi lakini moja ya maoni ni kuwa na benki ambayo itakuwa inatokana na Wanawake Wahasibu nchini na hilo watalitimiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...