KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imetangaza ujio wa chaneli ya watoto kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi chake. Chaneli ya StarTimes Kids itakuwa na chaguo la lugha ya Kiswahili kuanzia tarehe 10 Aprili mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja maudhui   wa Startimes Zamaradi Nzowa amesema kuwa chaneli hiyo ya ST Kids ni mahususi kwa ajili ya watoto wadogo wenye umri kati ya 5 hadi 9, na maudhui yake yanalenga kuwajengea watoto uwezo wa kuwa wabunifu na kuhusiana vizuri na wazazi wao.

Pia amesema kuwa,  "Kwa kuonesha tunajali ukuaji wa mtoto pamoja na utamaduni wa kitanzania, kwa sababu lugha ni sehemu ya utamaduni basi kuwa na vipindi vya watoto katika lugha ya Kiswahili itawasaidia kuwajengea kujiamini na kujifunza kwa urahisi zaidi kwa sababu ni lugha ambayo wanaielewa” Ameeleza Zamaradi.

 Aidha amesema kuwa ST Kids  ni chaneli ya kwanza ya watoto nchini ambayo vipindi vyake vitakuwa katika lugha ya Kiswahili hivyo ni nafasi ya kipekee kwa wazazi kuwapatia watoto wao kilicho bora kwa ajili ya ukuaji bora na amesema kuwa
Katuni ambazo zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ni pamoja  na ile inayopendwa zaidi ya paka wa Opera na  vipindi hivyo vitaanza kuoneka saa 12 jioni hadi saa 2 Usiku na vitakuwa vikirudiwa. 

Amesema kuwa mbali na katuni hizo pia kutakuwa na vipindi vingine vitakavyokuwa vikifundisha watoto mambo mbali mbali kama michezo, kuchora, kutengeneza maumbo pamoja na nyimbo.


Katuni na vipindi vingine vya Kiswahili vitaanza kuonekana saa 12 jioni siku ya tarehe 10 Aprili kwenye chaneli ya ST Kids ambayo inapatika katika kifurushi cha MAMBO kwa watumiaji wa dikoda za Antenna na kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda za Dish nchi nzima.
Muhamasishaji wa Mtandaoni Wema Sepetu akikikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano kwa niaba ya StarTimes Tanzania wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili leo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.
Muhamasishaji wa Mtandaoni Dinah Marious akikikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano kwa niaba ya StarTimes Tanzania wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili leo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.
Timu ya Idara ya Masoko StarTimes Tanzania na Wahamashaji wa Mtandaoni Dina Marious na Wema Sepetu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano mara baada ya uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili  leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili leo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...