Chama Cha mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kimetangaza majina ya waogeleaji wanne ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika katika mji wa Gwangju, Korea Kusini.

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro amewataja waogeleaji hao ni Hilal Hemed Hilal na Collins Saliboko ambao watashindana kwa upande wa wanaume ambapo kwa upande wa wasichana ni Sylvia Caloiaro na Shivani Bhatt.

Waogeleaji hao kwa sasa wapo katika maandalizi makali kwa ajili ya mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Julai 18 mpaka 29.

Hilal kwa sasa anafanya mazoezi Dubai kufuatia udhamini wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (Fina), nchini Dubai na Collins anajifua shuleni kwake, St Felix Uingereza huku Sylvia na Shivani wanatoka klabu ya Taliss-IST wanafanya mazoezi hapa hapa nchini.

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa aaogeleaji hao wamepata nafasi hiyo baada ya kukidhi vigezo mbalimbali vilivyowekwa.

Inviolata alisema kuwa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (Fina) litagharimia waogeleaji watatu na kocha mmoja katika mashindano hayo huku muogeleaji wanne atatakiwa kugharimiwa na chama husika kwa kupitia wadau wa mchezo.

“Waogeaji watatu, kocha na kiongozi wa TSA mmoja watagharimiwa na Fina. Waogeleaji watatu ni Hilal, Collins na Sylvia. TSA inaomba wadau kufanikisha safari ya muogeleaji wan ne ambaye ni Shivani ili naye kwenda kushindana,” alisema Inviolata.

Alisema kuwa waogeleaji hao kwa sasa wapo katika maandalizi kuelekea mashindano hayo ambapo Tanzania itakuwa inawakilishwa na waogeleaji wanne kwa mara ya kwanza.

“Waogeaji wetu wamepania kuhimarisha muda wao wa kuogelea ‘Personal Best time’ katika mashindano hayo ambayo ni makubwa sana duniani. Kutokana na hilo, wameamua kujiandaa vilivyo ili kufikia malengo yao na kupromoti mchezo kwa ujumla,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...