Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mhandisi Japhet Loisimaye akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kimbunga Kenneth ambacho kimesogea ukanda wa Kusini mwa Bahari ya Hindi na kwamba maeneo ambayo yataathariwa ni Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Kisiwa cha Mafia.

Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  limetoa tahadhari kwa Vyombo vya Majini kufuatia Kimbunga Kenneth kilichosogea ukanda wa Kusini mwa Bahari ya Hindi na kwamba  maeneo ambayo yataathariwa ni Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Kisiwa cha Mafia.   

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Japhet Loisimaye amesema Kimbunga hicho sio rafiki kwa Vyombo vya Majini kutokana na mawimbi yake kutembea kwa kasi ya KM 150 -      450 kwa Saa. 

Mhandisi Loisimaye ametoa tahadhari kwa Vyombo vidogo vya Majini kutokwenda majini, hata hivyo amesema Vyombo vikubwa  vichukue tahadhari kutokana na kuwa na vifaa vyenye uwezo wakuchukua tahadhari ya haraka.

‘’Vyombo vinavyofanya safari za Dar es Salaam – Zanzibar au Zanzibar – Dar lazima kuwa makini nakuchukua tahadhari zaidi vikiwa majini lakini hata Vivuko vyetu lazima vichukue tahadhari’’, amesema Mhandisi Loisimaye.  

Pia ameeleza kuwa kutokana na majukumu yao wanaowajibu wa kuhakikisha wanaotumia Vyombo vya usafiri wa majini wanakuwa salama na Rai kubwa Vyombo vidogo visiende kabisa majini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...