Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marukufu kuuzwa kwa nyaya za kupitia mawasiliano (Data Cable) zilizokuwa zikiuzwa kwenye baadhi ya maduka ya vifaa vya kielektroki baada ya kubainika hazikidhi viwango.

Hatua hiyo ilifikiwa na maofisa wa shirika hilo kwenye baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam baada ya sampuli za nyaya hizo kupimwa kwenye maabara na kudhibitika hazikidhi viwango.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mkaguzi wa TBS, Saimon Emmanuel, amesema tayari wenye maduka yaliyokuwa yakiuza nyaya hizo wamepewa muda wa siku 14 kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua.

Amesema baada ya kujiridhisha kuwa nyaya hizo hazikidhi viwango, hatua ya kwanza iliyochukuliwa ni kuzuia nyaya hizo kuendelea kuuzwa na ametoa mwito kwa Watanzania kutozinunua na kigezo kimoja wapo wanachoweza kutumia kuzitambua ni kuuzwa bei ndogo.

Pia amesema baada ya kupimwa kwenye maabara za shirika pamoja na kasoro nyingine, nyaya hizo zilibainika kuwa na kiwango kidogo cha madini ya shaba (copper) na kwamba hata nguvu kinzani kwenye nyaya hizo zilifeli kwenye maabara .

"Hivyo tumezizuia kwenye maduka tukisubiri hatua nyingine," amesema na kutoa mwito kwa wafanyabiashara wanapotaka kununua bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha zinakaguliwa ubora wake nje ya nchi kabla hazijaingia nchini mpangao ambao kitaalamu unaojulikana kama kama Pre-Shipment/Export Verification of Conformity to Standards (PVoC).

Pia ameongeza kuws wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi bila kukabuliwa kupitia PVoC, pindi bidhaa zao zinapofika nchini wanatozwa faini ya asilimia 15 kulingana na thamani ya mzigo, kulipia gharama za upimaji kwenye maabara na kwamba zinapofeli kufikia viwango muagizaji anaamuriwa kuzirudisha alikozitoa kwa gharama zake au kuteketezwa hapa nchini pia kwa gharama zake.

Emmanuel amesema hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Na:2 ya Viwango ya mwaka 2009. Ametoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha wazingatia sheria na taratibu ili kuepuka hasara.

Shirika hilo kwa sasa linaendesha awamu ya pili ya msako wa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni ili kubaini bidhaa ambazo hazina ubora na kuziondoa kwenye soko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...