Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV, Morogoro
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  Kanda ya mashariki imesema kuwa changamoto ya wananchi kukosa vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kusajili namba za simu kwa kutumia namba za vidole itatatuliwa na Mamlaka inayotoa vitambulisho hivyo (NIDA).

Changamoto ya vitambulisho hivyo imeibuka wakati Kanda ya Mashariki ilipokuwa inatoa elimu maeneo mbalimbali ya mkoani Morogoro kwa wananchi kuhoji vitambulisho vya taifa namna ambapo watavipata kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa muda uliowekwa kwa ajili ya usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole unafanya kila mwananchi atapata kitambulisho cha Taifa na kuweza kusajili laini kwa kutumia alama za vidole.

Aidha amesema kuwa baadhi ya watu walikuwa wanatumia simu ambazo zimesajiliwa na kwa majina ya watu wengine ambapo ni kosa kisheria. Amesema kuwa usajili wa laini kwa alama za vidole inaondoa mtu kumiliki laini kwa jina la mtu mwingine. Amesema kuwa katika kipindi hiki cha usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole kwa wenye vitambulisho wajisajili na wasiokuwa navyo wafuate utaratibu kwa kuvipata katika mamlaka husika kuweza kuvipata kwani mwisho wa kusajili ni Desemba 31 mwaka huu ambapo wasiosajili simu zao zitafungiwa.
 Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki  Robson Shaban akimpa maelezo mwananchi wa kijiji cha Mkuyuni.
 Mhandisi  Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Christopher John akitoa maelezo namna kutumia mawasiliano na umuhimu wa kusajili laini kwa kutumia alama za vidole wakati kanda hiyo ilivyokwenda kutoa elimu katika kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro.
 Wananchi wakipata elimu ya mawasiliano pamoja na usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole katika mnada wa kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Mkuyuni Mkoani Morogoro katika mnada wa kijiji hicho walipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano na Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Violet Eseko akitoa maelezo ya kisheria ya kumiliki simu zisizokuwa na majina yao wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi Mkuyuni mkoani Morogoro.
Mwananchi wa kijiji cha Mkuyuni akiuliza swali kwa TCRA Kanda ya Mashariki ilipokwenda kutoa elimu katika kijiji hicho.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na Abood Tv mara baada ya kumaliza kipindi cha utoaji elimu katika Radio Abood mkoani Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...