Na Hussein Stambuli, Morogoro..


Naibu katibu mkuu ofisi ya rais utumishi na utawala bora dr francis Michel amewataka viongozi wa umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuhakikisha wanawaondoa viongozi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi ambao wanakiuka katiba, miongozo na kanuni za vyama vyao badala yake wanaweka vipaumbele katika marumbano na migongano huku wakiacha kujadili mambo ya msingi kwaajili ya maendeleo ya wafanyakazi..

Akizungumza na kamati tendaji ya baraza kuu la shirikisho hilo katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadili na kuchambua jinsi ya kuboresha shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta, dr francis amesema viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanatakiwa kutambua wanajukumu la kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao wamewachagua na si masuala binafsi jambo ambalo litawafanya kupoteza wanachama wa vyama hivyo.

“ili kuachana na maslahi binafsi hakuna budi kwa viongozi kufuata katiba, miongozo na kanuni, sasa viko vyama ambavyo viongozi wao wanafanya vitu kwa maamuzi yao binafsi wakilala wakiamka anasema chama kitafanya hivi mara hii katiba haifai tubadili, mfumo huu unavuruga vyama watu wataondoka na chama kikikosa watu hakiendi na nikuombe rais na katibu mkuu tucta mnakazi kubwa si kuongoza tucta tu na kuongoza vyama kama kuna viongozi hawafai muwaondoe” amesema dr francis.

Aidha Rais wa umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamuhoka amesema licha ya serikali kuwa sikivu juu ya masuala mbalimbali ya wafanyakazi bado kuna wafanyakazi wa darasa la saba walioajiriwa tarehe 20 mei mwaka 2004 kwa baadhi ya maeneo wanakabiliwa na changamoto ya kutokurejeshwa kazini licha ya serikali kutoa tamko la kurejeshwa..

“baadhi ya maeneo watumishi hawa hawajarudi kazini na inatokana na tofauti kubwa iliyopo kati ya muajiri mmoja hadi mwingine, maeneo ambayo kunawatumishi waliojaza form za opras na wakajaza wamemaliza kidato cha nne na hawakujaza kwa mapenzi yao walijaza kwa kuelekezwa na maafisa utumishi kwasababu usipojaza kidato cha nne mfumo unakukataa kwasababu mfumo wa ajira serikalini unamtambua mtu mwenye elimu ya kidato cha nne na kukendelea kwahiyo baada ya kujaza fom hizo zimekuja kuwageuka leo wanaambiwa walidanganya baadhi ya halmashauri wamewakubali na baadhi wamewakataa” amesema rais tucta nyamuhoka.

Mwenekiti kamati ya wanawake tucta rehema ludanga amesema wanaishukuru serikali kwa kuwa sikivu hasa kwenye suala la vikokotoo na kuwaomba wafanyakazi nchini wanatakiwa kutambua shirikisho la tucta lipo kwa sababu yao na linafanyakazi kuwawakilisha wao.

“ningependa kuwaomba wafanyakazi nchini kutambua kuwa shirikisho linafanya kazi kwaajili yao na tunawaomba watuamini na tunaendelea kuwatendea kazi na tunashukuru kwa ushirikiano tunaoupata kutoka serikalini inaturahisishia kufanyakazi hasa mfano katika suala la kikokotoo ninaamini na mambo mengine yote yatakwenda vizuri” amesema rehema.
 Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Dkt Francis Michael akizungumza jambo kwenye mkutano huo
 Rais wa umoja wa shirikisho la vyama  huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamuhoka akizungumza na kamati tendaji ya baraza kuu la shirikisho hilo
 Umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadili na kuchambua jinsi ya kuboresha shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta,
Umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadili na kuchambua jinsi ya kuboresha shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta,_1

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...