Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akikabidhiwa zawadi ya akina mama wa UWT Jimbo la Mwanakwerekwe.
Kaimu Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Fatma Ramadhan akisoma risala ya UWT mbele ya Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma kondo katika ziara yake Wilayani humo.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akimkabidhi kadi ya uanachama wa UWT mwanachama mpya aliyejiuynga na umoja huo kutoka Chama cha ADA-TADEA ndugu Asha Juma Ali.
-Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akimkabidhi kadi ya uanachama wa UWT mwanachama mpya kutoka ADA-TADEA ndugu Dalila Hassan Sharif.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akizungumza na Wanawake wa UWT pamoja na viongozi mbali mbali wa CCM na jumuiya zake.
????????????????????????????????????
VIJANA wa Kikundi Maalum cha UVCCM wakimvisha sikafu Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Dimani Unguja,kwa ajili ya mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa Kamati ya Utekelezaji na Wanawake wa Wilaya hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akikagua Gwaride la Kikundi Maalum cha UVCCM mara baada ya kuwasili UWT Wilaya Dimani kwa ajili ya ziara yake Wilayani humo(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU YA CCM ZANZIBAR).
………………….
 
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 

WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kufuatilia mienendo ya watoto wa kike ili wapate malezi bora yatakayowaepusha na changamoto za udhalilishwaji wa kijinsia. 

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) anayefanyia kazi zake Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa Kamati tekelezaji ya UWT Wilaya ya Dimani kichama. 

Alisema wazazi,walezi na jamii kwa ujumla inatakiwa kuwa karibu na watoto wa kile ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira hatarishi ya kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji vinavyopelekea kuwakosesha haki zao za msingi zikiwemo elimu,uongozi na haki ya kuishi huru. 

Alisema wazazi wahakikishe watoto kila wanapotoka kwenda skuli na sehemu zingine za kijamii wakaguliwe mikoba yao kwani wengine wanaondoka na nguo za ziada na kwenda sehemu za starehe hali inayopelekea kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji. 

Alieleza kuwa jukumu la malezi ya watoto ni jukumu la kila mtu hivyo pindi watoto wakionekana katika mazingira hatari wananchi wa mtaa husika wanatakiwa kuchukua hatua za kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi ama kwa wazazi husika. Alibainisha kwamba kuna baadhi ya wanaume wasiokuwa na maadili mazuri wamekuwa ni chanzo cha kuwadanganya na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji watoto wa kike hasa wanaosoma shule za maandalizi na msingi,jambo ambalo ni kinyume na mila,desturi na utamaduni wa kizanzibar. 

Naibu Katibu Mkuu huyo Tunu, aliweka wazi kuwa CCM kupitia UWT Zanzibar itaendelea kulaani vitendo vyote visivyofaa vinavyokatisha malengo ya maendeleo ya wanawake nchini na kuishauri serikali ichukue hatua stahiki kwa wahalifu wote wa matukio ya udhalilishaji. 

Akizungumzia uimarishaji wa CCM Tunu, aliwataka Wanawake hao kulipa ada za uanachama kwa wakati ili kurahisisha mipango ya kiutendaji ya Chama na Jumuiya kwa ujumla. 

” Katubu Mkuu wetu juzi alininongoneza kuwa kuna mpango wa kuwapatia zawadi ya shilingi milioni moja (Sh.1,000,000),Katibu yeyote wa jumuiya ambaye Wilaya yake itaongoza kwa kulipa ada na kuongeza wanachama wapya kwa hiyo kazi kwenu”, aliwambia akina mama hao. 

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao,aliwasihi kuendelea kuongeza wanachama wapya na waliotimiza umri wa kupiga kura kisheria kwa lengo la kuongeza Jeshi la ushindi la CCM, litakalopambana vita ya kisiasaa na kukiletea ushindi Chama mwaka 2020. 

Pamoja na hayo aliwataka akina mama hao kuitumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa kuanzisha na kuendeleza vikundi mbali mbali vya kuzalisha bidhaa za ujasiriamali ili kwenda sambamba na malengo ya serikali ya kupiga vita wimbi la umaskini na utegemezi. 

“Wanawake tutaweza kufikia malengo yetu ya 50 kwa 50 endapo tutakuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mali na miradi mbali mbali ya kimaendeleo, wito wangu tuitumie vizuri fursa ya ujasiria mali itatukomboa kiuchumi”,alisisitiza. 

Katika maelezo yake Tunu, aliwasihi akina mama hao kuwakaribisha wanawake waliopo katika vyama vya upinzani ambao mpaka sasa wamekosa muelekeo wajiunge na CCM ili wanufaike na siasa na demokrasia iliyotukuka. 

Aliwapongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kasi yao ya usimamizi imara wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020. 

Amewapongeza akina mama hao kwa mapokezi mazuri yaliyoambatana na zawadi mbali mbali ambazo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano na umoja ndani na nje ya Chama na jumuiya. 

Akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi, Zainab Ali Maulid alieleza kuwa akina mama ndani ya Mkoa huo wanaendelea kufanya kazi za kuimarisha CCM ili itimize malengo yake ya kuendelea kuongoza dola. 

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani ndugu Hussein Ali Mjema ‘Kimti’ alisema Chama kitaendelea kuwa karibu na jumuiya zote kwa lengo la kuongeza nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo. 

Katika risala yao iliyosomwa na Kaimu Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Fatma Ramadhan Mandoba, alisema wanawake katika wilaya hiyo wameendelea kujikusanya pamoja na kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi. 


kupitia risala hiyo waliwashukuru baadhi ya Wabunge na Wawakilishi wa viti Maalum Wilaya hiyo waliotoa vitendea kazi mbali mbali vya kusaidia shughuli za kiutendaji za UWT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...