Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

UAMUZI wa maombi ya kutaifishwa kwa mali na fedha Sh.bilioni 14.1 za iliyokuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) kuwa mali ya serikali unatarajiwa kutolewa Mei 6, mwaka huu. Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia Jaji Stephen Magoiga kumaliza kusikiliza hoja za pande zote yaani ule wa Serikali na wa wajibu maombi.

Maombi hayo namba 42 ya mwaka huu yaliwasilishwa mahakamani hapo na Makurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga dhidi ya waliokuwa viongozi wa DECI Jackson Sifael Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Saiguran Ole Loitg’nye na Samwel Sifael Mtares.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, Dpp Mganga katika kuwasilisha hoja zake aliongoza jopo la mawakili watatu wa serikali, wakili wa Serikali Mkuu Poul Kadushi Teophil Mutakyawa na Shadrack Kimaro mawakili wa serikali.

Awali, wakili wa wajibu maombi, Majura Magafu alipinga maombi ya Dpp kwa madai kuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha kama fedha na mali zote za Deci zilitokana na michango ya wanachama (upatu).

Amedai, si kweli kwamba mali za Deci zilipatikana kwa njia isiyo halali kwani kampuni hiyo ilikuwa inafanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo watu kwa njia mbalimbali ikiwemo kuwapa mikopo.

Hata hivyo Magafu alipotakiwa kuonyesha  biashara zingine za deci kwa alishindwa kufanya hivyo kwa madai kuwa nyaraka zote zilichukuliwa na polisi wakati ofisi zao zilipovamiwa na kukamatwa wajibu maombi kipindi hicho.

Akiendelea kuwasilisha hoja zake, Magafu amedai, hakuna ushahidi wa  kutosha uliotolewa kuonesha kwamba hizi mali zilipatikana kwa njia ya ujanja ujanja,kitu walichokikubali wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali mahakama ya Kisutu  ni kuwa pesa ambazo zipo benki  kama viwanja  na magari vinàmilikiwa na Deci, hakuna sehemu yoyote waliyokiri kwamba mali zile zilipatikana kwa njia isiyo halalai.

Akijibu hoja hizo, DPP amedai kuwa fedha na mali hizo zimethibitika kuwa zilitokana na upatu na ndiyo maana Mahakama ya rufaa katika hukumu yake ilimuelekeza yeye kufungua shauri hilo Mahakama Kuu.

Amedai, Deci haikuwa na shuguli nyingine yoyote  mbali ya kukusanya fedha  na kwamba wajibu maombi hawakuleta ushahidi wa kupinga hilo hivyo   
biashara haramu ya upatu ndiyo ilikuwa kazi yao.

Kuhusu uhusiano wa mali za kanisa na Deci, DPP  amedai kuwa fedha zilizokuwa katika akaunti ya kanisa zilikuwa za Deci kwasababu wakàti huo hawakuwa na akaunti kwa kuwa walikuwa hawajasajiliwa.

Mapema, DPP,  aliwasilisha maombi mahakamani  akiiomba mahakama itoe amri ya kutaifishwa kwa mali za kampuni hiyo yakiwemo magari 11, nyumba na viwanja vinane na fedha ziwe nali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika maombi hayo, DPP anaiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kutaifishwa na kuwa mali ya serikali, nyumba namba UKMMD/1237 iliyoko Mwembe Madafu, Ukonga, Dar es Salaam, kiwanja namba 651, kitalu ‘M’ kilichopo Forest area, Mbeya, nyumba iliyoko kiwanja namba 7, kitalu ‘P’  ikiwa na hati namba  033004/23 kilichopo mtaa wa Rufiji, Manispaa ya Mwanza.

Mali nyingine ni ardhi iliyoko katika kiwanja namba 2/283/2 kitalu “E” Mabibo, Kinondoni, Dar es Salaam, kipande cha ardhi ambacho hakijapimwa kilichopo kijiji cha Manyinga, Turiani, Mvomero, Morogoro, kiwanja namba 467 kilichopo kitalu “H” kikiwa na hati ya usajili namba 48170 kilichopo eneo la Tegeta, Dar es Salaam, nyumba iliyoko kiwanja namba MM/19/P kilichopo Manzese karibu na barabara ya Morogoro, Dar es Salaam na nyumba iliyoko katika kiwanja namba KND/MXS/MNM/Z ikiwa na leseni ya makazi namba KND 008337 Kinondoni, Dar es Salaam.

Pia ameomba magari aina ya Toyota Premio lenye namba  T 132 AWJ, Toyota Land Cruiser namba T 480 AUP,   Toyota Rav 4 namba T 274 ATQ, Toyota Mark II namba T 676 AYP, Subaru Legacy namba T 682 AUT, Toyota Ipsum namba T 850 AXY, Toyota Ipsum  T455 ADM, Toyota Mark II T 186 AYX, Mitsubishi Pajero  T 852 AAV, Toyota Lande Cruiser T 789 AUX, Nissan Terrano namba T 899 AYU nayo yataifishwe na kuwa mali ya serikali

Pia, DPP anaomba kutaifishwa kwa fedha zilizoko benki katika akaunti namba 22601601056 iliyoko National Microfinance Bank (NMB), tawi la Msasani  ikiwa n ash. 12,503,068,647.89.

Fedha nyingine taslim ni zilizoko katika akaunti namba 000120100000194/1 iliyoko Dar es Salaam Community Bank (DCB), tawi la Uhuru ikiwa na sh. 1,457,700,462.49 na fedha taslim zilizoko katika akaunti namba 021140019558 iliyoko Kenya Commercial Bank (KCB), tawi la Samora, Dar es Salaam, ikiwa n ash. 57,933,304.10.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...