Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiwahutubia washiriki wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika Hoteli ya Leela Palace jijini New Delhi, India tarehe 26 Aprili 2019. Katika hotuba yake, Balozi Luvanda alieleza kuwa, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kihistoria na wa kupigiwa mfano duniani kote. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India ambao umedumu kwa miaka 58. 
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kushoto) kwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Paspoti, Visa na Diaspora wa (kushoto) na wageni waalikwa wakionesha jarida kuhusu miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa rasmi katika hafla hiyo. 
Mhe. Balozi Luvanda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Pasipoti, Viza na Diaspora wa India wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano. 
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali walioudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano. 
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...