* Watu milioni 900 wakiwemo vijana wajiandikisha kupiga kura, siku 38 zatengwa kwa kupiga kura

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

INDIA ina wapiga kura takribani Milioni 900(Ni Mara 18 zaidi ya Idadi ya watanzania wote) waliojiandikisha kwenye Time ya Uchaguzi.

Zoezi la kupiga kura litaanza tarehe 11 April hadi tarehe 19 Mei 2019, yaani takribani siku 38 kwa mizunguko 7 na kisha kura zitaanza kuhesabiwa tarehe 23 Mei 2019.

Waziri Mkuu wa sasa, Narendra Modi na chama chake cha BJP amerudi tena na kuomba kutetea tena kiti hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo, Sunil Arora, amesema kuwa uchaguzi utafanyika Aprili 11, mwaka huu na utawahusisha wapigakura milioni 900 na  kati yao wapiga kura milioni 15 ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 19.

Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, tatizo la uhaba wa ajira na kushuka kwa bei ya bidhaa za kilimo, vilishusha umaarufu wa Waziri Mkuu Modi, lakini wapigakura wanasema Chama Tawala cha  Bharatiya Janata Party (BJP), kitawapiku wapinzani wake baada ya mwezi uliopita jeshi la polisi la nchi hiyo kuingia vitani na wapinzani wa Pakistan hali inayoelezwa imewapa umaarufu zaidi na kuweza kupelekea  kujizolea mamilioni ya kura kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...