Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao wa  Hospitali ya Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa  siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu  ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri.

Kambi hiyo ni maalum kwa ajili ya  kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo hayo ambao bila ya kupata mtaalamu mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kuzibua mishipa hiyo wangefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

Matibabu hayo yanafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambapo mgonjwa anatobolewa tundu dogo katika paja ambalo linapitishwa vifaa maalum vya kuzibua mishipa ya damu ya moyo (Stent).

Katika kambi hiyo wataalamu wa afya wa JKCI watapata elimu ya jinsi ya kuzibua mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa.

Jumla ya wagonjwa 15 ambao mishipa yao ya damu mmoja hadi mitatu imeziba wanatarajiwa kutibiwa  katika kambi hiyo iliyoanza leo tarehe 23 hadi  25/4/2019. Hadi sasa wagonjwa watano wameshatibiwa na hali zao zinaendelea vizuri.

Imetolewa na:

Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...