Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa amewataka wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi kuhakikisha katika maeneo yao ya utumishi wanafanya kazi kwa uadilifu mkubwa na uzalendo kwa nchi yetu.

Ameshauri wahitimu hao waliomaliza mafunzo hayo katika Taasisi ya Uongozi wanakuwa mfano wa kuigwa katika maeneo yao ya utumishi kwa kuhakikisha mafunzo ya Uongozi ambayo wameyapata yanakuwa dira ya wao kutekeleza majukumu yao ya uongozi katika misingi ya kutenda haki huku akiwataka kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo ya pili ya Taasisi ya Uongozi jijini Dar es Salaam, Dk.Mwanjelwa amesema wahitimu wa mahafali hayo ya pili ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wanakilsababu ya kuonesha wameiva katika uongozi na kutekeleza majukumu yao katika kiwango cha kimataifa.

"Wahitumu mliopata mafunzo ya Uongozi kutoka hapa Taasisi ya Uongozi tambueni mnalo jukumu la kwenda kufanya kazi zenu kwa kutanguliza uadilifu na uzalendo mkubwa kwa Taifa letu.Kufanya kazi kwa umahiri peke yake haitoshi, hivyo hakikisheni mnafanya kazi kwa misingi ya maadili na uzalendo.

" Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu Dk.John Magufuli pamoja na mambo mengine inahimiza watumishi wa kada zote kuwa waadilifu katika maeneo yao ya utumishi.Hivyo kupitia mafunzo hayo tunaamini wahitimu ambao wengi wenu tayari ni viongozi huko mnakofanya kazi nendeni mkawe mfano wa kuigwa,"amesema Dk.Mwanjelwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Taasisi ya Uongozi kwa namna ambavyo imeamua kujiongeza kwa kuona haja ya kutafuta fedha ili kuhakikisha viongozi wanapata mafunzo hayo ambayo yanatija kubwa kwa Taifa katika kuandaa viongozi.

"Tunafahamu wapo viongozi ambao wanatokana na karama ya Mungu katika kuongoza lakini hiyo peke yake haitoshi kwani kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa amepikwa na kupata mafunzo ya uongozi kutoka kwa walimu wabobezi tulionao katika Taasisi ya Uongozi na wale wabobezi wa nje ya Tanzania.Hivyo mliohitimu leo hii niseme tu mmeiva na Taifa linawategemea ,"amesema Dk.Mwanjelwa.

Pia amewakumbusha watumishi wa umma na sekta binafsi wakiwamo wahitimu wa mafunzo ya Uongozi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kukomesha rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.

"Mafunzo ambayo mmeyapata mkayetende kwa kiwango cha kimataifa.Mmefundishwa maadili,vipaji,utawala bora,athar za rushwa na kuajiri. Hatutarajii kuona wahitimu wa mafunzo haya mnapokea rushwa na viongozi au kufumbia macho vitendo vya rushwa,"amesema.

Awali hotuba iliyotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa mgeni rasmi ilisema mafunzo hayo ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiama na Chuo Kikuu cha Aalto Finland yalizinduliwa Mei 19,2017 na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Anjellah Kairuki.

Mahafali ya kwanza yalifanyika Machi 21,2018 ambapo wengi wa washiriki walikua maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi la Tanzania. "Leo tunaazimisha mahafali ya pili, ambapo wahitimu wote pia ni maafisa waandamizi na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma. Mafunzo haya ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi yanachukua mwaka mmoja kukamilika, na yanatolewa kwa mfumo wa moduli.

" Mafunzo yana jumla ya moduli kumi, kila moja ikichukua mwezi mmoja kukamilika. Aidha, kila moduli inachukua siku mbili au tatu za darasani; na muda mwingine masomo hufanyika kwa njia ya mtandao. Kwa moduli zote, washiriki hulazimika kuhudhuria darasani bila kukosa, na kufanya mazoezi na mitihani yote. Kila mwanafunzi analazimika kufaulu mitihani na mazoezi yote ili atambulike kama mhitimu wa Programu hii na kupatiwa cheti,"imesema sehemu ya hotuba liyotolewa kwa mgeni rasmi.

Imeelezwa lengo la mafunzo hayo ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi ni kuwaimarisha washiriki katika maeneo makubwa matatu ya kiuongozi na kiutendaji.Maeneo hayo ni kuimarisha uwezo wao katika kufanya maamuzi ya kimkakati. Pia maamuzi ya kimaono, yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya sasa na ya baadaye kwa jamii.

Eneo jingine ni kuimarisha uwezo wao katika kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, ili kutekeleza kwa kikamilifu na kwa mafanikio maamuzi ya kimkakati, waliyoyafanya katika kipengele cha kwanza pamoja na kuimarisha uwezo wao katika kujijengea sifa binafsi za uongozi.

" Ni imani yetu maofisa Waandamizi na Viongozi hawa 34 ambao wametunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi watatumia sifa hizi walizozipata katika utekelezaji wa majukumu yao. Hata hivyo Programu hii bado ni changa. Kwa hivyo, pamoja na mafanikio tunayojivunia leo bado kuna changamoto.

"Kubwa ni ile ya gharama za kuandaa na kutoa mafunzo haya; gharama hizi ziko juu. Hili ni jambo la kawaida kwa Programu zote nzuri kama hii, ambayo pia inatambulika kimataifa. Wakati wa mahafali ya mwaka jana tulizungumza umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali kuchangia mafunzo haya. Hili tumejaribu kulitekeleza kuanzia awamu hii ya tatu,"imesema .
 Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliyekuwa mgeni rasmi katika.mahafali ya pili ya Taasisi ya Uongozi ( ) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na viongozi wa taasisi hiyo
 Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa akikabidhi cheti kwa mhitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi John Mongella ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza .Mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi katka mahali ya Taasisi ya Uongozi Dk.Mery Mwanjelwa ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akilishwa keki kama inashara ya wahitimu kutambua uwepo wake na ujumbe ambao ameutoa kwenye mahafali hayo
 Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa(hayupo pichani)
 Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali ya pili katika Taasisi ya Uongozi kushuhudia wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi

Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Uongozi na wafadhili wa mafunzo ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...