Na Rhoda Ezekiel Kigoma

WANANCHI wa vijiji vya Kagezi na Mlange wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita mbili kufuata maji katika Chanzo cha maji kutokana na mradi wa maji ulioghalimu zaidi ya Sh.bilioni moja kutokamilika tangu mwaka 2014 hadi sasa.

Wakizungumza jana kijijini hapo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani kwa baadhi ya miradi ya Serikali uliofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Serikali ya Wilaya hiyo, baadhi ya Wananchi hao waliokuwa wakigombania maji katika chanzo cha mto Kagezi, walisema wanapata shida ya kuchota maji na hasa ukizingatia kilima kilichopo katika chanzo hicho kinawachosha.

Agnes Kunjira ni mmoja kati ya wananchi hao alisema wanalazimika kuamka asubuhi kuwahi kuchota maji ndipo waende mashambani, kutokana na kero hiyo wanashindwa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa wakati kwa kuwa maji ni uhai na wanahitaji maji.

Aidha aliiomba Serikali kufuatilia kwanini mradi huo hautoi maji kwa kuwa kero waliyonayo inawatesa sana na endepo mradi huo ukikamilika na wakaanza kuchota maji vijijini itawasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha kagezi mwenyekiti wa Kijiji Zabroni Ntimba, alisema tangu mradi huo uanze kujengwa ni muda mrefu na mpaka sasa ulitakiwa uwe umekamilika lakini mwaka 2018 wananchi walipata maji kwa muda wa miezi mitatu tu na baada ya hapo maji hayakutoka tena.

Alisema wananchi wanalalamika kwani katika mradi huo walichangia asilimia 20 ya mradi hali hiyo inayosababisha kushindwa kuchangia hata shughuli zingine za maendeleo, kwa kuwa wamechangia mradi wa maji lakini hawaoni mradi ukifanya kazi.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo Mhandisi wa maji Wilaya ya Kibondo Michael Nguruwe alisema mkandarasi wa mradi huo aliingia mkataba ,wa Sh. 244,629,764, mradi ulitakiwa kuwa umekamilika 2014 lakini kutokana na changamoto ya fedha kulipa kwa wakati kwa mkandarasi mradi uliongezewa muda hadi 2018 lakini mpaka sasa haujakabidhiwa kwa wananchi.

Alisema tatizo kubwa lililopelekea mpaka sasa mradi huo kutokamilika kwa wakati, ni changamoto ya mfumo wa umeme, ambao mkandarasi alishindwa kuukamilisha na kama halmashauri wamezuia kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya umaliziaji wa mradi huo.

Alisema mpaka sasa wanaendelea kutafuta mkandarasi wa mfumo wa umeme katika mradi huo kwaajili ya kuweka kifaa kitakacho saidia kuongoza mfumo wa umeme katika mradi huo na mradi ukabidhiwe kwa Wananchi kwaajili ya kutumika.

Kutokana na changamoto zilizopo katika mradi huo na kero wanayoipata wananchi, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Hamisi Tahilo alisema Chama kinaagiza mradi huo kukamilika kwa kipindi cha mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja watafika katika mradi huo kuangalia kama kweli Wananchi wameanza kupata maji.

Alisema Serikali imetoa zaidi ya bilioni moja kwaajili ya mradi wa Wananchi lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika, Serikali iliahidi kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani ni lazima watendaji kuhakikisha Wanasimamia miradi ya serikali inafanyiwa kazi.

" Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM na fedha zinatopewa kwaajili ya kukamilisha miradi Wananchi wataiamini Serikali bqada ya kuona miradi hii inakamilika niombe ndani ya mwezi huo mmoja mradi huu uwe umekamilika", alisema Tahilo.

Aiwaomba wananchi kuwa na subira na kuendelea kujenga imani na CCM kwa kuwa imejipanga kuhakikisha wananchi wote wa vijijini na mijini wanapata huduma sawa sawa na wanaondokana na changamoto zote.
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kibondo wakiwasaidia Wannanchi kubeba maji.
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
 Kifaa kinachodaiwa kusababisha maji yasitoke katika mradi wa Maji kagezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...