Na woinde shizza globu ya jamii Arusha

Wanariadha nyota wa Tanzania  Alfonce Simbu na Josephy Panga ni miongoni mwa wakimbiaji mashuhuri ambao watashiriki katika mashindano ya Ngorongoro marathon  yanayotarajiwa kufanyika April 20 mwaka huu.
 
Wakimbiaji wengine nyota waliothibitisha kushiriki mashindano ni pamoja na Failuna Matanga,Anjelina Tsere ,Magdalena Shauri ,Fabian Joseph ,Faraja Damas pamoja na Natalia Elsante.

Akizungumza na Globbu ya Jamii leo muandaaji wa mbio hizo Meta Petro alisema kuwa mbio hizi ambazo zinafanyika kwa miaka 12 mfululizo zitashirikisha wakimbiaji zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi  wakiwemo wakimbiaji mashuhuri kutoka nchini Kenya.

Alisema mbio hizo zitakuwa za kilometa 21 ,kilometa tano pamoja na kilometa mbili na nusu kwa ajili ya watoto ambapo alitaja zawadi kuwa mshindi wa kwanza  wa kilometa 21 atapata milioni moja ,mshindi wa pili atapata laki tano ,na mshindi wa tatu atapewa laki tatu.

Alitaja malengo ya mbio hizo ni kupiga vita ujangili pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

"Unajua wananchi wengi na maanisha wa Tanzania wengi wamekuwa na tabia ya kutotembelea hifadhi zetu za taifa hivyo mbio hizi zitasaidia kuhamasisha wa Tanzania kuwa na tabia ya kutembelea hifadhi zetu" alisema Meta
  
Alisema  kuwa kwa washindi wa mita zote ambao watashika kuanzia Namba tano hadi kumi wao watapata fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama  ya Ngorongoro  kwa ajili ya kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Alitoa wito kwa wa Tanzania kujitokeza kushiriki mbio hizo .
Muandaaji wa Ngorongoro marathon akizungumza na Mwandishi wa habari hizi hii leo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...