Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Dawti la Jinsia la Wizara hiyo Lilian Ibengwe akizungumza na Wanawake wanaochakata Mazao ya uvuvi ni namna gani Serikali ilivyofungua fursa kwao katika dhana ya ushiriki na ushirikishwaji wa kurekebisha sheria mpya ya Uvuvi kwa kuwataka wanawake wa vuvi nchini kuweka maoni yao hili yaweze kuingizwa katika Rasimu ya sheria hiyo kwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserilakali la EMEDO, Editrudith Lukanga akizungumza namna ya shirika lake lilivyopambana kufanikisha kupatikana chama cha Wanawake Wavuvi nchini TAWFA na Hatimaye leo wanajadili rasimu ya sheria hili iweze kutambua haki za wanawake Wavuvi nchini.
Afisa Miradi kutoka shirika lisilo la kiserikali la Sea Sense Organisation, Emmanuel Mabula akieleza ni namna gani shirika lake lilivuojizatiti kumuinua Mwanamke Mvuvi nchini hili aweze kumiliki uchumi.
Mkurugenzi wa Sauti ya Wanawake Ukerewe, Sophia Donald akizungumzia Mikataba ambayo Taifa limeingia kusaidia kuleta usawa kwa wanawake bila ya kujali wanatoka katika sekta gani na kuwataka wanawake kuwa shupavu na kusimama kidete kutetea maslahi ya na taifa kwa ujumla
Sehemu ya Wanawake Wavuvi nchini ambao ni Wanachama wa TAWFA Wakisikiliza mada kutoka kwa wawezeshaji juu ya Rasimu ya Sheria ya uvuvi nchini na mazo yake.
Wanawake ambao ni Wanachama wa Chama Cha Wanawake Wavuvi Nchini wakiwa katika Picha ya pamoja wakati wa mkutano wa kujadili Rasimu ya sheria ya uvuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...