Picha ya pamoja ya washriki wa mkutano wa mafunzo kwa baadhi ya wataalam na wahandisi katika kilimo cha Umwagiliaji yaliyofanyika mapema jijini Dodoma leo.
 katika picha Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji na Matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Anthon Nyarubamba akiongea na wandishi wa habari hawapo katika picha kuhusu matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji
Katika Picha Mkurugenzi wa Idara ya Ufanisi na Utafiti kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Muyenjwa Maugo akiongea na waandishi wa Habari hawapo katika picha mara bada ya mkutano wa Mafunzo kwa wahandisi na wataalam katika eneo la kilimo cha umwagiliaji jijini Dodoma leo
katika picha ni Sehemu ya washiriki wa kikao cha mafunzo cha wahandisi na wataalam katika kilimo cha umwagiliaji kilichofanyika jijini Dodoma leo.



NA; MWANDISHI MAALUM - DODOMA

Imeelezwa kuwa Serikali kwa kushirikina na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan JICA kwa kupitia mradi wa kujengea uwezo wataalam nchini katika eneo la umwagiliaji imewapatia wahandisi na wataalam katika eneo la kilimo cha umwagiliaji mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo katika eneo la Mradi.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Usanifu na Utafiti Mhandisi Muyenjwa Maugo kutoka Tume ya Taifa ya umwagiliaji, ambapo Maugo alisema sambamba na hilo mradi pia umeendelea kutoa miongozo ikiwa ni pamoja na vitendea kazi vitakavyotumika katika ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji na upembuzi yakinifu ambapo ameeleza kuwa awali hakukuwa na muongozo katika skimu za miradi ya umwagiliaji jambo ambalo lilisababisha shughuli za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kutofanyika katika ubora unaostahili.

“Serikali inatumia rasimali nyingi kama vile fedha ili kuhakikisha miundombinu ya umwagiliaji inakuwa katika ubora unaostahili hivyo hatutaweza kuvumilia uendeshaji na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji usiofuata utaratibu na hatimaye kuwa chini ya kiwango.” Alisema Maugo.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji na Mtunzo Bw. Anthony Nyarubamba alisema kuwa Uelelimishaji katika eneo la utunzaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagilaji unaweza kuongeza tija katika eneo la uzalishaji wa chakula katika skimu nyingi za umwagiliaji nchini kwani muitikio kwa wakulima ni mkubwa mno. Akitolea mfano wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Igomelo Mkoani Mbeya ,Bw. Nyarubamba amasema kabla ya bei ya kitunguu kuharibika mkulima wa zao hilo alikuwa akipata takribani shilingi miloni Arobaini (40) kwa mwaka.

Aidha Bw. Nyarubamba amesema ili Nchi iweze kuingia vizuri katika uchumi wa Viwanda kilimo cha umwagiliaji kikitumika vizuri Nchi inaweza kupata malighafi za viwanda na kujipanga kulingana na masoko kutokana na upatikanaji wa mazao ya kutosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...