Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kililo Mkoani Iringa Philemon Namwenga  (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete, Wilaya Kilolo, mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani na wa kwanza kulia ni diwani wa viti maalum kata ya Idete Elina Kivegele na anayemfuatia ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.
 Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kililo Mkoani Iringa Philemon Namwenga (wa pili kulia) muda mfupi baada ya uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai  diwani wa viti maalum kata ya Idete Elina Kivegelea
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Philemon Namwenga pamoja na Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani, wakisalimiana na wananchi wa kijiji cha Idete Wilayani Kilolo mkoani Iringa muda mfupi baada ya uzinduzi wa manra mpya wenye uwezo wa 3G kijijini hapo.
Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani (wa pili kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Philemon Namwenga baadhi ya smart phone za gharama nafuu zinazouzwa na kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya uzinduzi wa mara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete wailayani Kilolo. Wa kwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.

Kampuni ya mawasiliano ya simu, Tigo, leo imezindua mnara wa 3G katika kata ya Kidete, mkoani Iringa kama moja ya jitihada zake za kufikisha huduma bora za kupiga na kupokea simu, intaneti na kutuma na kupokea pesa kwa wateja wake.
Akizungumza katika uzinduzi huo katika kata ya Idete, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi, aliwakaribisha na kuwashukuru Tigo kwa kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka teknolojia ya 2G hadi 3G.

Serikali ya Tanzania imefanya suala la viwanda kuwa agenda yake kuu. Na sisi kama serikali tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kufanikisha hii dira. Tunapenda kuwashukuru sana kwa kuifikiria Kilolo na wananchi wake, maana sekta hii ya mawasiliano ni chachu kubwa sana katika ukuaji na ubunifu wa viwanda mbalimbali,” alisema Kwezi. 

Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini, Abbas Abdurahamani, alisema kwamba kipaumbele ya Tigo ni kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma za kisasa za kiteknolojia za simu kama ya 3G.
Uzinduzi wa leo unaofanyika Kilolo ni mwanzo wa kampeni ya nchi nzima ambapo kutakuwa na uzinduzi wa minara 52 kutoka Tigo zitakazo zinduliwa kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini. 

Uzinduzi wa minara uaenda sambamba na ofa maalum. Wateja ambao watahudumiwa na minara ambayo imeongezewa uwezo kutoka 2G hadi 3G. Wateja watazawadiwa kiasi cha MB 100 za data kila mara watakaponunua kifurushi chochote cha intaneti. Huku wateja katika maeneo ya minara ya 4G itakayozinduliwa, watazawadiwa GB 4 za data bure pale wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G. 

“Kuongeza ubora wa mnara huu kutoka 2G kwenda 3G ina maana kwamba wateja wetu wa Kilolo sasa wataweza kupata huduma rahisi na kasi zaidi. Kwa mfano, 3G itaweza kuwapatia huduma ya intaneti iliyo bora ambayo itafungua jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Jambo hili litabadilisha namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Abdurahamani. 

Abdurahamani pia alisisitiza kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya Taifa na kuunga jitihada ya serikali katika viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbali mbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali. 

Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ukiondoa Kilolo zinapatikana katika maeneo ya Sumbawanga, Katavi, Mufindi, Njombe, Songwe, Mbeya and Songea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...