KUHARIBU MIUNDOMBINU YA UMEME.

Mnamo tarehe 01.04.2019 saa 23:00 usiku huko Kitongoji cha Mwaisongoli, Kijiji cha Mpunguti, Kata ya Ikama, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1. ELIA CHARLES [24] na 2. AMIR OMAR [27] wote vibarua wa Kampuni ya Umeme wa REA – STEG International Service na wakazi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa kuharibu miundombinu ya umeme.

Watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanakata nyaya za umeme za kampuni ya REA – STEG International Service kwa kutumia plaizi kwa lengo la kwenda kuuza ili wajipatie fedha. Thamani halisi ya uharibifu huo bado kufahamika. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

MAUAJI – MBEYA MJINI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawasaka watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AIDAN PAUL CHONGOLA [27] Mkazi wa Hayanga, Dereva Bodaboda.

Ni kwamba mnamo tarehe 03.04.2019 saa 02:00 usiku huko maeneo ya Ilomba, Jijini Mbeya, marehemu akiwa katika kituo chake cha kazi akiwa na Pikipiki yake yenye namba za usajili MC 557 BBT aina ya Kinglion rangi nyeusi alikodishwa na watu wawili wanaume wasiofahamika ili awapeleke Ituha lakini walipofika maeneo ya Ituha Relini watu hao walimchoma kitu chenye ncha kali upande wa kulia tumboni na kusababisha kifo chake na kasha kuondoka na Pikipiki hiyo.

Mwili wa marehemu ulikutwa kando kando ya reli ya Tazara, Mtaa wa Tonya April, 03, 2019 saa 07:00 asubuhi ukiwa na jeraha tumboni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu. Aidha msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili kwa hatua zaidi za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...