Waziri wa Uwekezaji, Angellah Kairuki akizungumza wakati ufunguzi wa mkutano wa majadiliano kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania na China uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.

Na Khadija Seif, Globu ya jamii

SERIKALI imetoa pongezi kwa Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke kwa namna ambavyo ameendelea kujenga ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo sekta ya uwekezaji.

Pongezi hizo zimetolewa leo Aprili 17,2019 na Waziri wa Uwekezaji Angellah Kairuki wakati ufunguzi wa mkutano wa majadiliano kati ya  wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mbali ya wawekezaji na wafanyabishara, pia mkutano huo umehusisha taasisi, kampuni za kibiashara pamoja na maofisa wa wizara mbalimbali ambazo zinahusika na mambo ya biashara na uwekezaji.
Kairuki wakati anazungumza kwenye mkutano huo amesema "Nampongeza pongezi Balozi wa China nchini Tanzania kwa kuendelea kuamini nchi ya Tanzania na kutengeneza ushirikiano mzuri baina ya nchi mbili hizo katika kila nyanja ya kimaendeleo ,"amesema Waziri Kairuki.
Ameongeza  umoja wa jamii ya watu wa China uliopo nchini umewezesha kuwekwezwa kwa Dola za Marekani bilioni saba ambazo kwa sehemu kubwa zimewanufaisha Watanzania huku akifafanua  wapo raia wa China ambao wameamua kuifanya Tanzania sehemu ya makazi yao ya kudumu.

Waziri Kairuki amesema mikutani ya aina hiyo itaendelea kufanyika na huo ni mwanzo tu kwani pamoja na jamii hiyo ya Wachina kuwekeza katika nchini Tanzania na kutengeneza baadhi ya bidhaa na kufanya biashara bado wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upatikanaji wa vibali na hivyo kusababisha malalamiko madogo madogo.

Kwa upande wake Balozi Wang Ke ametoa pongezi kwa Rais Dk.John Magufuli kwa kuendelea kuwakaribisha raia wa China kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.

Balozi Ke amesema mbali na mkutano huo kujenga ushirikiano wa kibiashara, pia utasaidia kutoa ujuzi kwa wawekezaji wa nchini zingine akitolea mfano Watanzania wenyewe kujaribu kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia ujuzi utakaotolewa na Wachina.
Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Daniel Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari.

"Tunafahamau mshikamano uliopo baina ya nchi ya China na Tanzania unafanya nchi hizi mbili kuendelea kushirikiana kwa hali na mali japo changamoto hazikosekani ,"amesema Balozi Ke.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Damas Daniel Ndumbaro amesema ushirikiano wa nchi hizo mbili utaendelea kuimairishwa kwani ni muhimu katika kukuza maendeleo ya Watanzania.

Dk.Ndumbaro amesema nchi ya China imeshaonesha utayari wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kujenga urafiki  katika biashara,uchumi na kukuza teknolojia nchini.
Balozi wa China nchini Tanzania Wang ke akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungua mkutano wa wawekezaji kati ya nchi ya China na Tanzania jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...