Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.  Angela Kairuki ametoa wito kwa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Tanzania (ATAPE) na wawekezaji wengine wazawa kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na kusajili miradi  yao ya Uwekezaji katika Tume ya uwekezaji ya Taifa (TIC).

Kairuki ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 20 wa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Tanzania (ATAPE) Mjini Bariadi, ambapo amebainisha kuwa kwa mwaka huu 2019 wawekezaji wazawa zaidi ya asilimia 72 wamesajili miradi yao ya uwekezaji TIC.

“ Kwa mwaka huu peke yake tumepata wawekezaji wazawa waliosajili miradi yao ya uwekezaji TIC zaidi ya asilimia 72, hii inanipa faraja sana kama waziri wa nchi ninayesimamia uwekezaji ninapoona Watanzania wenzangu wanachangamkia fursa”

"Naomba mchangamkie fursa hizo kwa sababu wawekezaji wa nje tunapenda waje tu endapo watakuja kuungana nasi kwenye mtaji, kubadilishana nasi ujuzi na uzoefu " alisema Kairuki.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara, uwekezaji na kuweka vipaumbele kwa ajili ya kuvutia wawekezaji katika sekta ambazo zitakuwana athari na tija kubwa kiuchumi kwa wananchi, ili kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo,uvuvi, na mifugo ambayo ni maeneo yanayoajiri Watanzania wengi zaidi.

Aidha, Waziri Kairuki amezitaja sekta nyingine za kipaumbele kuwa ni  uzalishaji wa mafuta ya kula kwa kutumia mbegu zinazozalishwa nchini, uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa dawa za binadamu, vifaa tiba na kemikali, ujenzi wa miundombinu ya uvuvi wa kisasa, viwanda vya kuchakata samaki, kusindika nyama, viwanda vya kubangua korosho, viwanda vitakavyotumia pamba na viwanda vya  pembejeo na mbolea.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ameipongeza ATAPE kwa jinsi  inavyoshirikiana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji pamoja na huduma nyingine.

Kairuki amesema serikali pekee  haiwezi kutatua changamoto zote hivyo  kwa kushirikiana na wadau ikiwemo taasisi za dini wanaweza kuwahudumia wananchi na kuleta mabadiliko chanya ikiwa ni pamoja na  kuhubiri amani, huku akisisitiza kuwa masomo ya ujasiriamali yanayotolewa kwa wana ATAPE wayatumie kwa manufaa ya kanisa na jamii kwa ujumla.


Awali akimkatibisha waziri Kairuki, mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkutano huo umewasaidia  watu wa  Simiyu  kukutana na watu wa maeneo mengine hatua iliyopelekea kubadilishana uzoefu  sambamba na kuongeza na kupata masoko mapya .

‘’watu wetu wameongeza wigo wa masoko, mmebadilishana uzoefu ....huu ni mkoa wa kibiashara na ni mkoa wenye fursa nyingi;  tunajenga tawi la chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) hivyo ninawaalika wafanyabiashara na Watanzania wote kuja kuwekeza ujenzi wa hosteli eneo lile linalojengwa tawi hilo"alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ATAPE Freddie Manento amesema kwa miaka mitatu ATAPE imewekeza miradi ya bilioni 1.2 katika miradi yenye manufaa kwa kanisa, wanajamii na wana ATAPE.

Alisema wamewekeza kwenye miradi ya maji kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa, miradi ya miti ya matund), korosho na miradi ya mashamba ya mihogo kwa kutengeneza ajira na faida katika vijiji walivyolima mashamba yao.

‘’Wana ATAPE wamejitoa kwelikweli na wameitikia dhana yetu ya kutumia vipaji na rasilimali zetu kwa ajili ya kazi ya MUNGU, hii iko katika mathayo 28;19, 20…hii ndio dhana yao’’ alisema Manento.

Mkutano wa Wanataaluma na Wajasiriamali (ATAPE) kutoka kanisa la Waadventista Wasabato umefanyika mkoani Simiyu kwa muda wa siku sita ambapo umehudhuriwa na wananchama zaidi ya 1500.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi
 Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi
 Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), Bw. Freddie Manento akimtambulisha rasmi  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki (mwenye skafu) kama mwanachama mpya mbele ya wanachama, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho Mjini Bariadi
 Kutoka kushoto Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki, Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati(nchi 11) , Mchungaji Emanuel Pelote, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Mchungaji Joshua Njuguna kutoka nchini Kenya, wakifurahia jambo wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),  hicho Mjini Bariadi
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka(mwenye shati la Kitenge kushoto) akiimba pamoja na wanakwaya ya Bulka kutoka Jijini Arusha, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),  hicho Mjini Bariadi
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akionesha ngao/tuzo alichopewa na Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),   kama shukrani ya kuwezesha mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho kufanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho Mjini Bariadi
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la Kaskazini , Dkt. Godwin Lekondayo akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...