Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif akionyesha wateja waliotembelea katika banda hilo.
Mmoja wa mtendakazi katika kampuni hiyo akionyesha aina ya mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira wataanza kuisambaza kwa wananchi kwa bei nafuu.


Na Vero Ignatus, Kilimanjaro

Wazalishaji wa mifuko mbadala wametakiwa kuchangamkia fursa kuzalisha mifuko kwa wongi ya kukidhi mahitaji ambayo ni rafiki wa mazingira kwani tayari mkoa wa Kilimanjaro umeshapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira alipotembelea maonyesho ya wiki ya elimu katika uwanja wa Mashujaa Wilayani Moshi ,amesema kuwa wajasiriamali wanaotumia vifungashio vya mifuko ya plastiki wanapaswa kujiianda mpaka muda uliopangwa na serikali Mwezi June mwaka huu waweze kuondokana na matumizi ya plastiki.

“Kwa sasa mkoa wa Kilimajaro ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki tumeanza mapema ili watu wajiandae ikifika mwezi wa sita mwaka huu watu wawe kwenye mstari na kuzoea kutumia mifuko mbadala tunashukuru wenzetu wa Harsho Group wameanza kuzalisha mifuko ya kutosha ” Alisema Dkt.Anna

Nae Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro wamejianda vyema kuzalisha mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira na kuisambaza kwa bei nafuu.

Caroline alisema kuwa wanazalisha mifuko laki 5 kwa siku ambayo inatosheleza mahitaji ya mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani pamoja na Tanzania nzima hivyo wamejiandaa kuzi ba pengo la mifuko ya plastiki.Anaeleza kuwa mifuko hiyo inaweza kufuliwa zaidi ya mara tano na iwapo ikitupwa inaweza kuoza na kuwa mbolea katika ardhi.

Mkazi wa Manispaa ya Moshi Roman Mnzava alisema kuwa hatua ya Mkoa wa Killimanjaro kupiga marufuku matumizi ya plastiki utasaidia kuokoa mazingira na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni kitovu cha utalii mkoani hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...