Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano na Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaack Nchunda wakionyesha bango baada ya  ya Airtel kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’, huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando. 
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya Airtel kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’, huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaack Nchunda.



· Punguzo Pekee kutoka Airtel, uhuru wa kuongea

· Airtel sasa yawezesha wateja kupiga simu mitandao yote kwa 1TZS bila bando 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuwapa wateja wake huduma kabambe na za kipekee ikiwa ni jibu na itikio la mahitaji ya wateja wao kwa kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’, huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando.

Huduma hii mpya ya TAMBA MITANDAO YOTE inakuja wakati muafaka na kuwapa wateja wa Airtel uhuru wa kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa punguzo la kiasi cha 1TZS tu kwa kila sekunde hata kama mteja hajajiunga na bando au kuishiwa bando.

Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuthibitisha kuzinduliwa kwa huduma hiyo ya TAMBA MITANDAO YOTE kwa niamba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema ‘Tunayo furaha kubwa kuzindua huduma hii ambayo inawapa wateja wa Airtel uhakika wa kupiga simu kwenda mtandao wowote hapa nchini kwa gharama nafuu ya 1TZS kwa sekunde, tunaamini kupitia Tamba Mitandao Yote mteja wetu ataona thamani ya pesa yake na kufurahia uhuru wa kuongea wakati wowote. 

 Nchunda aliongeza kuwa wateja wa Airtel watafurahia pia punguzo la vifurushi vya intaneti kutoka TZS172 kwa MB mpaka TZS40 kwa MB ikiwa hajajiunga na bando lolote, pia mteja atafurahia kutumia TZS10 tu kwa MB ikiwa mteja alikuwa na kifurushi cha bando ambacho hakijaisha muda wake huku punguzo la gharama za ujumbe mfupi zikishuka kutoka TZS 69 kwa kila ujumbe mpaka TZS 10 kwa kila ujumbe’.

”TAMBA MITANDAO YOTE” ni huduma ambayo inampa mteja wa Airtel huduma bora, huru na nafuu kwani hata kama mteja atakuwa hajajiunga na bando yoyote bado anaweza kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa gharama ndogo ya 1TZS kwa sekunde. Tunaamini hii ni hatua kubwa sana kwenye sekta ya mawasiliano ambapo vikwazo vyote vimeondolewa na kuwapa Watanzania unafuu wa kupiga simu bila kujali kipato chake,’ alisema Nchunda.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘Kulingana na taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya wateja wanaotumia simu za mkononi kwa kupiga kati ya mwaka 2017 na 2018 imeongezeka kutoka milioni 40 mpaka 43. Idadi ya wateja wetu imeongezeka pia kwa kipindi cha robo mbili za mwaka uliopita na hii imetokana na hudumu zetu zenye ubunifu na unafuu wa hali ya juu. Tunaamini huduma yetu itawawezesha wateja wetu kupata uhuru wa kupiga na kuongea ,wakiokoa fedha zao na kuziweka kwenye maendeleo ya kiuchumi. 

Airtel imekuwa mstari wa mbele kwenye kuleta huduma nafuu na zenye ubunifu ambazo zinakidhi matakwa ya wateja wetu kama vile huduma za kifedha, SMS, kupiga simu na hata kwenye huduma za intaneti.

‘Airtel inaendelea kukuza wigo wa mtandao wake nchini ambapo kwa sasa tuna maduka ya Airtel Money Branches zaidi ya 650 ambapo mteja anaweza kupata bidhaa na huduma mbalimbali kama za kifedha, kuunganisha kwenye vifurushi vya intaneti pamoja na kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole’, aliongeza Singano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...