Na Ali Issa Maelezo -Zanzibar 

Ujumbe wa wanafunzi sita kutka Chuo Kikuu cha Harvad umefanya mazungumzo na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Ofisini kwake Migombani.

Ujumbe huo upo Zanzibar kuangalia ubora wa chumvi inayozalishwa hapa nchini ukilinganisha na mataifa mengine ili hatimae iweze kutambulika na kuingia katika soko la kimataifa.

Akizungumza na Ujumbe huo Balozi Amina Salum Ali amesema Chumvi inayozalishwa Zanzibar ina ubora wa hali ya juu kutokana na mfumo unaotumika wakati wa uzalishaji na inaweza kutumika katika nchi yoyote duniani.

Amsema kufika kwa ujumbe huo ni mafanikio kwa mradi wa chumvi ya Zanzibar na ameeleza matarajio yake kuwa utasaidia kuhakikisha chumvi ya Zanzibar inaingia katika soko la kimataifa.

Aliutaka ujumbe huo kufanya uchunguzi wa kina kujua ubora wa chumvi ya Zanzibar na kuona tofauti iliyopo na chumvi inayozalishwa n nchi nyengine duniani.

Mbali na kuangalia ubora wa chumvi inayozalishwa Zanzibar, pia ujumbe huo utakagua kilimo cha pilipili na kilimo cha mwani ambacho kimekuwa maarufu sana katika maeneo mbali mbali ya pwani ya Zanzibar.

Wanafunzi hao kutoka Marekani wametawanywa katika mataifa mbali mbali na kwa hapa Tanzania wamekuja kumi ambapo wanne wamebakia Tanzania Bara.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Ujumbe wa wanafunzi sita kutoka Chuo Kikuu cha Harvad cha Marekani Ofisini kwake Migombani, wanafunzi hao wapo nchini kuangali ubora wa Chumvi inayotengenezwa Zanzibar.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali na ujumbe wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Harvad wakiangalia Paketi za Chumvi iliyotengenezwa Zanzibar Ofisini kwake Migombani.Picha Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...