Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini wanaendelea na harakati zao za kufutari pamoja zinakopelekea kushibana kiimani ya moyo ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao umeteremshwa Kitabu Kitakatifu cha Quran kisichoshaka katika kubainisha Haki na Batil.

Futari hizo zinazojumuisha Waumini wa rika tofauti ufanywaji wake hupaswa kuzingatia utaratibu maalum wa hali ya Kiafya na Mazingira safi uliowekwa na Uongozi wa Manispaa pamoja na Halmashauri za Wilaya.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi iliwahusisha Wazee wanaohifadhiwa kwenye Nyumba za Serikai Sebleni pamoja na Wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na kufanyika katika Ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Mjini Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed alisema Balozi Seif bado anaendeleza tabia njema ya kuwashirikisha Wananchi mbali mbali katika Futari ya pamoja.

Waziri Aboud alisema kitendo cha kufutarisha ni maamrisho ya Mwenyezi Muungu aliyoawaagiza Waumini wake wenye uwezo kuwasaidia Waumini wenzao wenye maisha duni ili kuwaunganisha katika futari hiyo ambayo ni matendo anayoyafurahia Allah Subuhanahu wataala.

Mjumuiko wa kufutari kwa makundi ni utaratibu aliyojipangia Balozi Seif wakati anapopata wasaa wa kufanya hivyo katika muelekeo wa kuwashirikisha Wana Jamii kwenye mjumuiko huo wenye kuleta ushirikiano miongoni mwa Wananchi mbali mbali Nchini.


 Baadhi ya Wazee wanaoishi katika Nyumba za Serikali Sebleni Mjini Zanzibar waki katika Futari ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa shukrani kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mara baada ya futari ya pamoja na Wazee wa Nyumba za Serikali Sebleni.
 Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wazee Wanaume wanaoishi nyumba za Serikali Sebleni mara baada ya kufutari nao pamoja iliyowashirikisha pia baadhi ya Wazee wa Chama Mkoa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wazee Wanawake wanaoishi nyumba za Serikali Sebleni mara baada ya kufutari nao pamoja iliyowashirikisha pia baadhi ya Wazee wa Chama Mkoa Kaskazini Unguja. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...