Basi la kampuni ya Fikoshi linalofanya Safari zake kati ya Karagwe na Mwanza limegonga tembo usiku wa kuamkia leo katika eneo la Byenturege Kitengure Wilayani Karagwe lilipokuwa likitokea Mwanza. 

Sehemu hiyo ni Sehemu ya Lunch na ipo chini ya NARCO, pia MTU mmoja ndiye kajeruhiwa kufuatia ajali hiyo Nafuatilia namba za gari na Jina la majeruhi 

Eneo hilo ni Sehemu ya Ranchi ya wanyama ambayo ipo chini ya NARCO ambapo Wanyama tofauti kama Swala, Simba, Tembo ambao hupenda kukatiza Barabara wakati wakijitafutia chakula, licha ya kuwepo kwa alama na Vibao vya Tahadhali, lakini Magari yamekuwa yakipita kwa kasi katika eneo hilo na inaelezwa ndio sababu ya basi hilo kugonga Tembo. Hakuna binadamu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo zaidi ya Tembo na Basi kuumia. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi hapo baadae.
 Basi la Fikoshi linalofanya Safari zake kati ya Karagwe na Mwanza limegonga tembo usiku wa Jana  eneo la Byenturege Kitengure Wilayani Karagwe likitokea Mwanza. Hakuna madhara mengine zaidi ya Basi kuumia. Tunaendelea kufuatilia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...