Dodoma. Benki ya NMB wamekubali kusaidia wakulima wa zao la zabibu mkoani Dodoma,ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali wa kuwainua wakulima.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NMB Albert Jonkergouw katika hafla fupi ya benki hiyo kwa taasisi za serikali, viongozi wa taasisi na wafanyabiashara iliyofanyika katika ukumbi wa new Dodoma hotel.Mkurugenzi huyo alisema nguvu kubwa imeelekezwa kwa wakulima kutokana na sera ya Tanzania ya viwanda lakini akasifu mpango wa serikali kuhamia Dodoma ambao umeungwa mkono na benki hiyo.

Jonkergouw alisema katika kuunga mkono uhamiaji Dodoma, NMB wameshapeleka tawi la benki tembezi katika mji wa kiserikali Mtumba na kwamba mipango ya baadae ni kufanya maboresho makubwa ya huduma za benki katika eneo hilo.

“Tutaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara, mimi niseme kuwa benki hii ni mali yenu mna haki ya kuitumia nasi ni wajibu wetu kuwahudumia,” alisema Mkurugenzi.

Akizungumza katika halfa hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge aliomba uongozi wa NMB kuutazama mkoa wa Dodoma kwa jicho la pekee kutokana na ongezeko la watu kufuatia ujio wa makao makuu.

Dk Mahenge aliomba benki kurahisisha masharti katika upatikanaji wa mikopo ikiwemo kuwapa kipaumbele zaidi wakulima wa zabibu zao linalotajwa kuwa mkombozi kwa wenyeji w amkoa huo.

Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamini Mkapa ya Jijini hapa Dk Alfonce Chandika alisema benki ya NMB ni rafiki kwa makundi yote kutokana na huduma zake kuyagusa makundi yote.

Dk Chandika alisema kwa sasa huduma zinazotolewa na benki hiyo zinapaswa kuwa mfano kwa taasisi zingine jambo litakalotoa tafsiri chanya kwa Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Albert Jonkergouw akiongea na watumishi wa Serikali na wafanyabiashara kwenye chai ya Asubuhi iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma jana. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR. Binilith Mahenge (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Albert Jonkergouw (Kulia) kwenye chai ya Asubuhi iliyo andaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...