Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo, akifungua mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika Chuo hapo Mei 25, 2019. Mafunzo hayo yalitolewa na wanafunzi wanaosomea chuoni hapo kwa wajasiriamali wadogo.

Mratibu wa mafunzo ya wajasiriamali, Yusuph Zuberi.

Dk. Godbertha Kinyondo (kulia), akifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa kwa wajasiriamali wadogo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Washiriki.

Zuberi Kopwe akitoa mada kuhusu Masoko na Mkakati wa Kimasoko.
Raphia Kimaro, akitoa mada kuhusu Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo, Huduma kwa Wateja na Utunzaji Kumbukumbu.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wajasiriamali Malkia Wajane, Sophia Samfundo, akielezea namna alivyonufaika na mafunzo hayo hasa suala la kufanya biashara mtandaoni.

Mfanyabiashara wa bidhaa za ngozi akizungumzia changamoto anazokutananazo katika biashara yake.

Mjasiriamali akiuliza swali.

Mjasiriamali akiuliza swali.

Brenda akijibu maswali ya baadhi ya wajasiriamali.

Ben Shine, akitoa mada kuhusu Masoko Kidigitali 'Digital Marketing'.

Hozza Mbura akitoa mada kuhusu Fursa.

Washiriki.

Hozza Mbura akijibu maswali.

Baadhi ya washirikia wakifuatilia mafunzo hayo.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Nela Alam, akifunga mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo ya ujasriamali wakiwa katika picha ya kumbukumbu na wakufunzi wao.
Picha ya kumbukumbu ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali.

Picha ya kumbukumbu ya wakufunzi wa mafunzo hayo.



Na John Marwa


WAJASIRIAMALI wadogo nchini wameaswa kutobaki nyuma katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kukuza biashara zao na kuongeza faida.

Hayo yalibainishwa na watafiti wa Sayansi ya Jamii na Masoko kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, katika Semina ya Mafunzo ya Masoko kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki.

Semina hiyo ilibeba dhima ya kuwajengea uwezo na kukuza uelewa wa wajasiriamali wadogo katika kulifikia soko na kupata faida.

Miongoni mwa mada zilizotolewa na Wandaaji wa Semina hiyo ambao ni wanafunzi wa chuo hicho ni matumizi ya mitandao katika kuwafikia wateja, Digital Marketing,

Akizungumza katika Semina hiyo mtoa mada wa Masoko Kidigitali Ben Shine aliwaomba wajasiriamali wadogo kuchangamkia fursa ya kidigitali ili kukuza biashara zao na kuweza kuwafikia wateja ili kutengeneza faida.

"Katika kukuza biashara zetu ama huduma kama wajasiriamali wadogo hatupaswi kubaki nyuma katika Masoko Kigitali (Digital Marketing) ili kuwafikia wateja.


"Sababu kubwa ya kutumia Masoko Kidigitali ni kutangaza bidhaa au huduma ili watu waweze kuzifahamu, kutoa taarifa juu ya biashara na huduma zako katika jamii,, alisema Ben na kuongeza kuwa.

"Jambo lingine baada ya kutangaza biashara zetu na kupata wateja ni kuweza kuziuza ili kutengeneza faida.


Bena alisema kuna mitandao ya kijamii mingi hapa nchini hivyo kila mjasiriamali anapaswa kujiunga huko ili kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi katika kukuza Biashara.


Kwa mfano kupitia Barua pepe, Blog, Kurasa za Kijamii, Facebook, Instagram, WhatsApp pamoja na Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii inayotumiwa na watu wengi zaidi hivyo kuwa njia rahisi ya kuwafikia wateja na kutengeneza wapya.

Mada nyingine iliyofundishwa katika Semina hiyo ni Masoko au Soko ikiwa ni shughuli yoyote anayoifanya mfanyabiashara ili kukizi mahitaji ya mteja na kupata faida.


Akidadavua mada hiyo mtoa mada Zuberi Kopwe alisema katika soko Mfanya Biashara ama Mjasiriamali ni kutambua uhitaji wa mteja ili kutengeneza faida.


,,Ili kulifikia soko inatupasa kutekeleza malengo ya biashara au huduma husika kisha kufanya tathimini ya kila jambo lililoko mbele ya biashara ama huduma yako.


"Utaratibu wa kumfikia mteja kwanza ni kufanya tafiti ili kumfahamu mteja, pili mteja anataka nini, pia kuuliza kujua mahitaji ya mteja" alisema.


Kopwe aliongeza kuwa katika Biashara kuna Bidhaa au Huduma, bei ya kuuzia, njia bora ya kuwasiliana, mwonekana wa Mazingira, watu au wafanya kazi wenye kuvutia wateja na mwisho vyote humjengea mteja Imani ya Bidhaa zinazozalishwa au huduma.


Katika hatua nyingine wajasiriamali walipata nafasi ya kujifunza jinsi gani ya kukua katika biashara mada iliyotolewa na Raphia Kimaro.


Kimaro aliwataka wajasiriamali kufahamu sifa na tabia ya kuwa mjasiriamali. Moja ni kutafuta mwanya au nafasi ya kufanyia biashara.

"Miongoni mwa sifa na tabia za mjasiriamali ni kujiamini, utashi wa kutambua ubora wa bidhaa au huduma, uthubutu wa kufanya mambo, ushawishi kwa wateja, malengo yenye kutafsiri muelekeo wa biashara".


Zingine ni uwezo wa kusimamia biashara, kutafuta taarifa au habari juu ya biashara au huduma ili kujifunza jambo jipya, lakini pia ubunifu ni sehemu pekee ambayo humuongezea mjasiriamali ubora wa bidhaa au huduma katika ushindani wa soko" alisema Kimaro na kuongeza kuwa.


"Mjasiriamali ni Mfugaji na sio Mwindaji kwa maana ya tabia, kwani mfugaji huweza kukuza mifungo vivyo hivyo mjasiriamali anapaswa kukuza biashara yake, lakini Mwindaji yeye hutumia kilichopo chote na sio mkuzaji.


Nao wajasiriamali waliohudhuria Semina hiyo walitoa kongore zao kwa wandaaji na kutoa rai ya kuendelea kupewa fursa ya kupata mafunzo juu mambo mbali mbali yanayoendana na sekta ya ujasiriamali.


"Kiukweli tuna kila sababu ya kuwashukuru hawa vijana wetu kwa kuweza kutujali hasa sisi wajasiriamali wadogo".



"Kuna mengi tumejifunza hasa suala la kufanya biashara mtandaoni ni jambo ambalo binafsi nimelifurahia sana na naimani kama tutalitumia vema basi tutaweza kupiga hatua" alisema Sophia Samfundo Mwenyekiti wa kikundi cha Wajasiriamali Malkia Wajane kutoka Pugu Kajungeni.


Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi Dk. Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo, alisema Wajasiriamali ndio nguzo ya uchumi hivyo wanapaswa kutambua nafasi yao katika kukua kwa uchumi wa nchi "Tanzania ya Viwanda ni nchi ya Wajasiriamali, tunaweza kufanya mambo makubwa tukiwa wabunifu, weledi wenye kujituma huku tukimtanguliza Mungu kwa kila jambo" alisema Kinyondo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...