Na Khadija Seif, Michuzi TV

KAMPUNI  ya KC Land Development Plan imesema imejipanga ili kuweza kuwasaidia wananchi waishio katika hali ya chini Viwanja kwa bei rahisi, na imeahidi kuwapatia wasanii ambao ni wanachama wa Uzalendo Kwanza viwanja kwa ajili ya kumiliki ardhi na kupata makazi.

Akizungumza na waandishi wahabari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Khalid Mwinyi amesema, wamefikia uamuzi huo lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Mwinyi amesema kwa sasa utoaji wa Viwanja hivyo utaanzia  mikoa ya Dar es Salaam, Pwani pamoja na  Dodoma na kwamba malipo yatakuwa ni kwa mwaka mmoja hadi miwili. Ametoa rai kwa wasanii wa Bongofleva pia kumiliki viwanja hivyo kwa bei  ambayo anahisi kila msanii ataweza kumudu kulipia.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Uzalendo Kwanza Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere ameshukuru kampuni hiyo kwa kuwaona kwenye jambo hilo muhimu na kuwapa kipaumbele. Amesema anaamini sifa kubwa kama msanii ni kumiliki Kiwanja, ambapo amemshukuru Mkurugenzi wa KC na kusema kuwa jambo hilo limekuja kwa wakati sahihi.
 "Nikweli wasanii tumekuwa tukitangatanga katika nyumba za kupanga tunawashukuru KC kwa kutuona na kutuwezesha kupata ardhi kwa kuwa heshima ni kuwa na nyumba na si gari, kaulimbiu yetu ni Maisha ni nyumba"alisema Steve. 
Aidha Kampuni hiyo imejipanga kufanya hafla ya chakula cha jioni katika ukumbi la Lamada siku ya mei 5,2019 lengo likiwa ni kuwaweka pamoja wasanii na kujadiliana nao jinsi ya upatikanaji wa viwanja hivyo na jinsi gani wataweza kuwa mabalozi wa wananchi na kuwahamasisha kumiliki viwanja vyao.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya KC Land  Khalid Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...