Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akikambidhi kadi ya CCM aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kwembe Manispaa ya Ubungo, Dweza Horace Kolimba (Chadema) leo jijini Dar es Salaam. 
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kwembe Manispaa ya Ubuongo, Dweza Horace Kolimba (Chadema) na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Liberata Samson, wakionyesha kadi zao chama chao kipya cha CCM leo. 
Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akizungumza na vijana wa CCM Wilaya ya Ubungo, wakati wa uzinduzi wa Ubungo ya Kijani Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala akizingumza katika mkutano wa Kampeni ya Dar ya Kijani, jijini Dar es Salaam leo 
Vijana wa hamasa wa Manispaa ya Ubuongo, wakishangilia jijini Dar es Salaam leo. 
……………… 
 
Na Ripota Wetu-Michuzi TV 
 
KAMPENI ya Dar es Salaam ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), imewang’oa Diwani wa Kata ya Kwembe Dweza Horace Kolimba (Chadema) na Katibu wa Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Liberata Samson kwa kujiunga na CCM. 

Akiwapokea wanachama hao leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde, amesema mwaka 2020 ni lazima majimbo mawili la Ubungo na Kibamba yarudi ndani ya mikono ya CCM. 

Mavunde amesema kuwa hiyo ni dalili tosha kwamba CCM watachukua majimbo hayo na ni aibu kuyaacha majimbo hayo mawili yakiwa upinzani. 
Amesema kama makosa yalifanyika hapo awali hategemei tena kurudia tena na majimbo hayo yakaachwa chini ya John Mnyika (Kibamba ) na Saed Kubenea (Ubungo), kwa kuwa hakuna wanachokifanya zaidi utekelezaji wa ilani ya CCM unafanywa na wao. 

“Kama kuna uhitaji wa maji, barabara nzuri vyote vinafanyika sasa kuna haja gani ya kubakia upande wa pili wa upinzani ni lazima vijana kufanya kazi kuhakikisha majimbo yanarudi CCM na katika uchaguzi wa serikali za mitaa kata zote ziwe chini ya chama hicho. 

“Jitahidi hapa viongozi hii ni aibu anzeni na mitaa yote 91 kuhakikisha inarudi CCM mana hapa nikiangalia hakuna hata pa kupita Mnyika wala Kubenea watapitia wapi,” amesema Mavunde na kuhoji. 

Amesema jukumu la chama cha siasa ni ushindi na kushika dola na ili ushinde ni lazima kuishi matatizo ya wanajamii sasa kwa serikali ya sasa imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za wananchi wake. 
Hata hivyo amesisitiza kuwa Rais Dk. John Magufuli anakubalika ndani na nje ya nchi huku akitolea mfano, alipokuwa Afrika Kusini juzi wakati wa kuapishwa Rais Cyril Ramaphosa, ambapo alishangiliwa na wananchi wananchi wan chi hiyo. 

Katika hatua nyingine Mavunde amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii, kujiajiri wakati wakisubiri mchakato wa serikali katika kuongeza ajira kwa vijana hao. 

Amewataka kuhakikisha wanakuwa katika vikundi vya ujasiriamali vya kukopeshana ili waweze kupata fedha kwani Ubungo ina fedha nyingi ambazo zimetengwa kwa ajili yao waweze kukopeshwa na kujiendeleza. 

Katika hatua nyingine aliwapongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha kampeni ya Dar ya Kijani kwa kupandisha bendera ya CCM kila kata. 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema wanashirikiana vizuri na viongozi wa majimbo ya Ubungo lakini bado watahakikisha kata zote 14 na majimbo ya Wilaya ya Ubungo zinarejea CCM kwani ziliazimishwa kwa muda. 

“Jimbo la Ubungo na Kibamba lazima yachukuliwe na CCM mwaka 2020, hakuna sababu ya kubaki upinzani kwani Rais Magufuli anafanya mambo makubwa ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla. 

“Na hii kampeni ya Dar ya Kijani itaambatana na kazi ya kutundika bendera, ufunguzi wa matawi kwa kila kata za Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020. Hivyo ni jukumu letu vijana kujipanga na kuhakikisha tunarejeasha heshima ya chama chetu CCM,” amesema Kilakala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...