Na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango amelishauri Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), kuweka namna bora ya kuingiza ajenda ya uwekezaji kwa watoto katika mikutano mbalimbali inayofanyika Barani Afrika.

Hayo ameyasema alipokuwa akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman, anayehamia nchini Kenya.

Dkt. Mpango alisema Shirika hilo linatakiwa kuweka mkazo huo ili kuhakikisha nchi za Afrika zinaweka mipango ya kuwekeza kwa ajili ya watoto kwa kuwa kundi hilo ndiyo Taifa la kesho.

Alisema Serikali ya Tanzania kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Elimu Nchini, imekuwa ikitoa kipaumbele katika elimu kwa kutoa elimu ya awali, msingi na sekondari bure kwa lengo la kutoa nafasi kubwa kwa watoto ili wapate haki yao ya msingi.

Aidha Dkt. Mpango alisema kuwa katika kuboresha Sekta ya Elimu Duniani ni vema pia masuala ya lishe bora kwa mtoto yakatiliwa mkazo kwani lishe bora inachangia afanye vizuri dararasani lakini pia itamsaidia mtoto kuwa na afya bora itakayomfanya aweze kufikiri vizuri.

“Nitahakikisha agenda za kulinda haki ya mtoto nchini inapewa kipaumbele kwenye mikutano yetu mikubwa tunapokuwa tukijadili masuala ya maendeleo kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Mpango.

Aliongeza kuwa jukumu la kumlinda mtoto ni la kila mmoja kwakuwa wote walishawahi kuwa watoto hivyo ni vema kila mmoja atomize jukumu hilo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Tanzania Bi. Maniza Zaman, anaye hamia nchini Kenya, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanya nae kazi vizuri kwa kipindi chote alichokaa nchini.

“Tanzania ni nchi nzuri, watu wake wana upendo, wana utu na wakarimu karibu kwa mikoa yote 19 hadi 20 niliyowahi kutembelea wakati wa kutekeleza majukumu yangu”, alisema Bi. Maniza.

Alitoa wito kwa Serikali, kuendelea kutoa kipaumbele kwa ajili ya Sekta ya Elimu na Afya kwa kuongeza angalau asilimia moja ya bajeti kila mwaka kwakua zimekuwa na changamoto nyingi kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu kila siku.

Pia aliiomba Serikali ibuni mbinu na kuweka mipango endelevu kwa ajili ya watoto itakayowasaidia katika siku zijazo kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa takriban watoto milioni 2 huzaliwa kila mwaka.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango alimuahidi aliyekuwa Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman, kuwa Wizara yake itaendelea kuhakikisha Sekta hizo zinapata bajeti ya kutosha katika mgawanyo.

Dkt. Mpango amemshukuru kwa kufanya kazi nchini na kumkaribisha tena na tena hasa kipindi cha mapumziko ambapo amesema milango ipo wazi muda wowote atakapojisikia kutembelea Tanzania.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza wakati wa kuagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bi.  Maniza Zaman, anayehamia nchini Kenya, alipokwenda kumuaga ofisi kwake, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akisisitiza jambo wakati wa kuagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bi.  Maniza Zaman (hayupo pichani), anayehamia nchini Kenya, alipoenda kumuaga Waziri wa Fedha na Mipango ofisini kwake, Jijini Dodoma.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayehamia nchini Kenya Bi.  Maniza Zaman, akizungumza wakati alipokwenda kumuaga Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (wapili kulia), wa kwanza ni Kamisha Msaidizi Idara ya Bajeti Dkt. Charles Mwamwaja, wakati wa kikao cha kuagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) anayehamia Kenya, Bi.  Maniza Zaman, (hayupo pichani).
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi.  Maniza Zaman akifurahia jambo alipokwenda kumuaga Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, ofisini kwake (hayupo pichani), wapili ni Mwakilishi wa UNICEF anayeshughulikia Sera za Jamii Bw. Paul Van Ufford Dodoma.
 Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (wapili kulia), wa kwanza ni Kamisha Msaidizi Idara ya Bajeti Dkt. Charles Mwamwaja (kushoto), kulia ni Ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), ukiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika  hilo nchini anayehamia nchini Kenya  Bi.  Maniza Zaman, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipokea zawadi yenye picha ya watoto kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Tanzania Bi.  Maniza Zaman, anayehamia nchini Kenya alipokwenda kumuaga ofisini kwake, Jijini Dodoma.
aziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akifurahia zawadi yenye picha ya watoto aliyopokea kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) aliyehamishiwa nchini Kenya, Bi.  Maniza Zaman alipokwenda kumuaga ofisini kwake Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...