Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wahitimu na wananchi waliohudhuria mahafali ya 30 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Kaimu Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel Shindika akitambulisha makundi ya wahitimu wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Charles Msonde akitoa neno la utangulizi wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi bora waliohitimu Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakiwa mbele ya meza kuu mara baada ya kukabidhiwa vyeti na zawadi wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) na baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.


Wahitimu wa mahafali ya 30 wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wametakiwa kuwa waadilifu, wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Dkt. Mwanjelwa alipokuwa akiwatunuku vyeti wahitimu hao katika mahafali yaliyofanyika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kampasi ya Mtwara.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, waajiri wote nchini wanatambua umahiri wa utendaji kazi wa wahitimu wanaotoka Chuo cha Utumishi wa Umma, hivyo amewataka wahitimu hao kuendelea kujenga taswira nzuri ya chuo kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, sasa ni wakati muafaka kwa wahitimu hao kuonyesha utofauti wao kiutendaji na wahitimu wengine ambao hawakupata fursa ya kusoma Chuo cha Utumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza wahitimu hao, kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa wabunifu katika utendaji kazi ili kukidhi mahitaji ya wananchi na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anaiishi kwa vitendo kaulimbiu yake ya HAPA KAZI TU.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewakumbusha wahitimu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukizwa ambayo yanahatarisha nguvu kazi yao kwani elimu na maarifa waliyoyapata yatakuwa hayana maana, iwapo watashindwa kuyatumia kutokana na matatizo ya kiafya ambayo yanaepukika. Kutokana na umuhimu wa mafunzo yanayotolewa na chuo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa msisitizo, ametoa rai kwa waajiri wote nchini kuendelea kukitumia Chuo cha Utumishi wa Umma kuwajengea uwezo watumishi wa umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hii, kuwaasa watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii, na amewaonya kutojenga makundi ambayo kimsingi yatakwamisha utendaji kazi na maendeleo ya chuo kwa ujumla.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Charles Msonde amesema bodi ya taaluma ilipitia kwa kina taarifa za matokeo za wahitimu wote na kujiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa, wanastahili kutunikiwa vyeti.

Dkt. Msonde amesema, waajiri mbalimbali wamethibitisha kwamba, wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wamekuwa ni bora kiutendaji katika maeneo yao ya kazi na kuongeza kuwa, ni lengo la chuo kuwaandaa wanafunzi wote wanaopata mafunzo TPSC kuwa lulu katika soko la ajira.

Awali, Kaimu Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel Shindika amewataka wahitimu kuitumia elimu waliyoipata kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla, na amewapongeza waelekezi katika kampasi zote kwa kuwapa mafunzo bora wahitimu hao, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchango wake katika kukiboresha chuo hicho.

Jumla ya wahitimu 2686 walitunukiwa vyeti vya awali, astashahada, stashahada na shahada ya uzamili katika fani za Utunzaji wa Kumbukumbu, Uhazili, Sheria, Menejimenti ya Rasilimaliwatu, TEHAMA, Utawala wa Umma, Manunuzi na Ugavi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...