Fainali ya Mavunde Cup kata ya Kikuyu Kaskazini imemalizika jana kwa kishindo kikubwa kwa Timu ya Kikuyu Football Club kuibuka kidedea na kunyakua ubingwa huo baada ya kuitandika Timu ya St John’s University kwa bao moja kwa bila katika Mchezo uliochezwa katika Viwanja vya Chuo kikuu cha St John’s na kuhushuriwa na maelfu ya wananchi wa Dodoma.

Akihitimisha mashindano hayo,Mfadhili wa mashindano hayo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amezipongeza timu zote kwa ushiriki wao na kuonesha uwezo mkubwa wa vipaji vikubwa kwa muda wote wa mashindano na kuahidi kwamba atahakikisha anaendelea kuvikuza na kuvilea vipaji hivyo ili Vijana hao pia waweze kufikia malengo yao katika mchezo wa mpira wa miguu ambao sasa umekuwa ni fursa ya Ajira kwa Vijana wengi.

Akishukuru kwa niaba ya Vijana wenzake,Mratibu wa mashindano hayo *Comrade Elibariki **alimshukuru Mbunge Mavunde kwa Ufadhili wa mashindano hayo na vifaa vya michezo kwa Timu *10 ambazo zimeshiriki katika mashindano haya lakini pia na namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Vijana katika Jimbo la Dodoma Mjini katika nyanja mbalimbali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...