Na Mwandishi wetu, Tandahimba 

Viongozi wa Serikali za vijiji na vitongoji katika Tarafa ya Mihambwe wilayani Tandahimba wametakiwa kuelewa dhana ya utumishi na uongozi ni dhamana ya wananchi si mwanya wa kujitajirisha au kuonea wengine kinyume na sheria.

Pia viongozi na wajumbe wa kamati za Serikali wametakiwa kuheshimu kanuni na sheria za nchi kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Msimamo huo umetolewa na Katibu tarafa ya mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu alipombana Mwenyekiti wa Kijiji cha Namunda (CUF) Suleiman Kazumari Mkubulu kufuata madai ya upotevu wa mifuko 24 ya saruji.

Shilatu aliwaelekeza viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji kuelewa kiongozi asiyeheshimu taratibu za kiutawala ajiweke Kando kabla hajashitakiwa Kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Midhali Mwenyekiti umekiri kimaandishi mbele ya Serikali ya Kijiji na Kamati ya ujenzi, Nakutaka urudishe mifuko ya saruji 24 kabla ya Mei 30, 2019. Chochote kinacholetwa vijijini na Serikali Kuu au Halmashahuri ya wilaya ni mali ya umma." Alisema Gavana Shilatu

Alimtaka Mwenyekiti huyo kutimiza ahadi yake kama alivyohaidi kimaandishi kabla hatua nyingine zaidi hazijachukuliwa kisheria dhidi yake." Alisema Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu alishangazwa na matumizi ya shilingi Milioni 12 fedha ambazo hazilingani na hali halisi ya gharama za ujenzi wa miradi ilivyo.

"Kiasi kikubwa cha fedha hapa kimetumika tofauti na miradi ilivyo. Kamati ya ujenzi ifuatilie kwa kina kujua matumizi kama yanafanana na gharama ya fedha za mradi" Alieleza.

Katika ziara hiyo Gavana huyo alikagua miradi ya maendeleo ya kijiji hicho akiambatana na Wajumbe wa kamati nzima ya Serikali ya Kijiji cha Namunda.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...