Na.Khadija seif,Globu ya jamii

MKONGWE wa tasnia ya Michezo ya kuigiza nchini Chausiku Salim a.k.a Bichau ameliomba  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuchuja na kuzifanyia uhakiki filamu zinazooneshwa kwa sasa kutokana na nyingi kukiuka maadili ya kitanzania hasa kwa wasanii wa kike.

Akizungumza na Globu ya Jamii Bichau amesema kwa sasa nyimbo nyingi zimekua zikifungwa kutokana na mashairi kutumia lugha zisizo na maadili na kupelekea kuvunjika kwa mmomonyoko wa maadili, amesema bodi ya filamu ndio muhimili mkuu katika kuweka vibali na Kuruhusu kazi za filamu kuoneshwa hivyo ni wakati wa kuweka vibali huku swala la maadili likizingatiwa na kupewa kipaumbele zaidi.

"kufanyia uhakiki filamu hizo kutokana na nyingi kukiuka maadili na kusababisha mmomonyoko kuvunjika siku hadi siku na kusababisha kuzalishwa kwa vijana wa hovyo, wenye tabia zisizofaa kutokana na kuigwa igwa huku wasanii wakiwa kama kioo cha jamii"

Aidha Bichau ameeleza wasanii wengi hawathamini mchango wa watu waliowafikisha walipo, japo jitihada zao binafsi zilitumika kupelekea kujulikana na kuzuka kwa mitafaruku isiyo na tija wala faida katika kukuza na kufanya mapinduzi ya tasnia na kusababisha mabishano na majivuno kwenye kazi ndio chanzo cha migawanyiko na matabaka na wasanii kutoshirikiana kwenye kazi.

"Wanajitahidi kufanya tasnia kukua zaidi kutokana na teknolojia kukua lakini ni wazi tasnia imetekwa na uzungu na tamaduni za nje huwezi kutazama filamu ukiwa na watoto ama wazazi ni aibu tupu "amesema bichau

Hata hivyo Bichau amesema kwa sasa amepumzika kwenye sanaa kutokana na kufanya kazi kwenye kituo kimoja cha redio nchini na lakini yupo tayari kwa yeyote mwenye kutaka ushauri,mawazo na hatosita kumsaidia.

Bichau ameweka wazi kuwa hatotokea msanii mwenye kipaji kama marehemu Mzee small mungu ampe kauli thabiti na kila mwaka humfanyia dua kwa ajili ya kumbukizi kama shukrani kutokana na yeye kuchangia kufika hapa alipo.

Ametoa rai kwa wadau na makampuni nchini kutopendelea kwa baadhi ya majina ya wasanii hasa likija swala la kupewa kazi ama tuzo kwani hata wakongwe Wanaweza kufanya kazi ipasavyo kutokana na sanaa ni ajira yao,wanaendesha maisha yao kupitia sanaa.
Bi Chau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...