Na, Editha Edward-Tabora.

Uhaba wa Miundombinu ya madarasa,viti,meza katika shule za msingi, Halmashauri ya  manispaa ya Wilaya ya Tabora, unatajwa kurudisha nyuma jitahada za  ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.

Hayo yamebainishwa mapema hii leo na mkuu wa Wilaya ya  Tabora Manispaa,Erick Komanya wakati akipokea mifuko 200 ya Saruji kutoka shirika la Reli Tanzania Mkoa wa Tabora (TRC).

Komanya amesema tatizo hili la uhaba wa madarasa linayumbisha jitihada za ufaulu kwa vijana walioko mashuleni huku akiwahakikishia  wadau wote wanaotoa michango yao ili kuinua Elimu  katika Halimashauri ya Wilaya ya  Tabora Manispaa kuwa michango hiyo itafanya kazi iliyokusudiwa.

"Madarasa 128 ambayo tumekusudia kuyajenga kwa mwaka huu, kila kata katika Halimashauri ya Manispaa ya Tabora inatakiwa kuhakikisha inajenga vyumba vinne (4)vya Madarasa" amesema Komanya.

Akizungumza na Michuzi Blog  Kwaniaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Bwn Kadogosa Masanja,mkuu wa chuo cha Reli mkoani Tabora ndugu John Kaberege,huku akikabidhi mifuko 200 ya saruji amesema shirika limeamua kufanya hivi ikiwa ni moja ya kufanya kazi ya jamii  Coorparate Social Responsibility(CSR).

"Shirika la Reli mkoani Tabora tumeamua kuchangia mifuko hii ya saruji ili kutengeneza mazingira mazuri ya Elimu kwa watoto wetu ambao ni viongozi wa kesho" amesema Kaberege.

Hatahivyo Halimashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Tabora bado inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya Madarasa zaidi ya 230 ikiwa mahitaji ni vyumba 360 na tayari vyumba 128 vimeshaingizwa kwenye mpango wa Ujenzi, hali hii inapelekea baadhi ya wanafunzi kukaa kwa kubanana na  kushusha kiwango cha Ufaulu wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...