Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo ambapo IGP Sirro aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akinunua matunda kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo kwa lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajasiliamali ndogo ndogo katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, IGP Sirro yupo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa ajili yake wakati alipowasili katika Kituo Kikuu cha Polisi wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia Kitta, wakati alipowasilia wilayani humo kwa ziara ya kikazi yeye lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...